Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA) wakiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius
Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA) wakiangalia bidhaa mbalimbali za uchongaji na ushonaji toka
kwa wajasiriamali wa Tanzania kabla ya kuanza kwa kikao cha shirikisho hilo
mapema hii leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere
(JNICC), jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni
Infantino (katikati) akiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini
Dar es Salaam, kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika Ahmad Ahmad
na kulia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Wallace Karia.
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni
Infantino (aliyevaa shuka la kimasai) akivalishwa urembo wa mkononi wenye rangi
za bendera ya Taifa mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema
hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano Mkuu toka Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB) Geofrey Tengeneza (kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino, zawadi mbalimbali toka bodi hiyo kabla ya
kuanza kwa mkutano wa shirikisho hilo mapema hii leo katika Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment