Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw Charles Kazungu Akitoa msaada kwa Bi, Teddy Saidi wakati wa zoezi la kutoa misaada katika kuadhimisha miaka 41 ya chama cha mapinduzi Wilayani Geita. |
Baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi wakiwa wameambatana na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw Charles Kazungu wakitoa msaada kwa mtoto Zuberi Juma. |
Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw Charles Kazungu akitoa msaada kwa Bw,Fredy Magunga. |
Katibu wa chama cha mapinduzi(CCM)Julius Peter akitoa pole kwa mgojwa ambaye alikuwa kwenye wodi ya wakinamama Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Geita. |
Consolata Evarist.Geita
|
Zoezi hilo
limeendeshwa na uongozi wa chama na baadhi ya wanachama wakiambatana
na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa ambaye alikuwa ni mgeni Rasmi ,Bw
Charles Kazungu alisema maamuzi ya kutembelea hospitali ya mkoa ni kutaka
kujua namna ambavyo ilani ya chama hicho inavyotekelezwa kwenye sekta ya
afya.
Aidha
ametoa wito kwa watumishi wa Sekta hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia
taratibu na sheria ambazo zimewekwa na nchi.
“Natoa wito kwa watumishi ambao wanatabiaya
kutokutoa huduma vizuri kwa wagonjwa kuachana na tabia hiyo rai yangu
waweze kutimiza adhima na kazi zao utawala wa chama cha mapinduzi hususani
awamu ya tano unataka wafanye kazi kwa mujibu na sheria nasi vinginevyo”,
alisema Kazungu
Kazungu
alisema katika kuhakikisha serikali inajali wananchi wake imeonelea ni
vyema maadhimisho kwa ngazi ya wilaya wakayafanyia hospalini na kutoa
msaada wa kuwasaidia watu ambao wanauwitaji maalumu kama wagonjwa.
Pia
amewataka wananchi kufika katika vituo vya afya kwani vimeboreshwa kwa
kiasi kikubwa na vina hudumia kwa umakini mkubwa hivyo wasipendelee kukaa na
magonjwa nyumbani wanaweza kusababisha vifo na matatizo makubwa ambayo yange
weza kuzuilika.
kwa upande
wake katibu wa umoja wa wazazi Wilaya ya Geita,Happynes James ameiasa
jamii pindi inapopata matatizo ya kiafya ni vyema wakafika kwenye vituo vya
afya ili kujua ni matatizo gani ambayo yanawasumbua na kuachana na dhana ya
kukimbilia wa waganga wa kienyeji
Baadhi ya
wagonjwa akiwemo Teddy Mathayo na Juma Mabeyo wameishukuru serikali pamoja na
chama cha mapinduzi (CCM) kwa msaada ambao wameutoa kwa moyo walio uonesha
wakuonesha kujali na kuwafariji kwa kiasi kile walicho balikiwa na kwamba
wamefarijika sana kwa tukio hilo .
No comments:
Post a Comment