Mwenyekiti wa mtaa wa Shinde Bw,Makoye Mirambo akizungumza juu ya uharibifu huo unavyowaathiri wananchi wake.
Wananchi wa mtaa wa Nshinde
Wilayani Geita wamelalamikia ubovu wa barabara inayoelekea fadhiri bucha na
mwatulole kuwa kero kubwa kutokana na ubovu ambao umekuwa
ukisababisha gari nyingi kukwama na kukosekana kwa baadhi ya huduma za usafiri.
Akizungumza na mtandao huu Bi Fatuma mwita amesema tatizo hilo ni
la muda mrefu na bado halijapatiwa ufumbuzi jambo ambalo linapelekea
usumbufu katika harakati zao za kutafuta maendeleo na kwamba wamekuwa wakipata
shida pindi hususani mvua zinaponyesha.
Aidha ameongeza kuwa wamekuwa wanapata usumbufu mkubwa kutokana na
kuwepo mashimo katika barabara hiyo na kupelekea baadhi ya madereva kukataa
kupita na wengine hali ambayo imeendelea kusababisha kuendelea kuharibika
kwa barabara.
“Inafika wakati watoto wanashindwa kwenda
shule kutokana na ubovu huu wa barabara jamani yani huku sisi tumekuwa kama
tupo kisiwani ambapo akuna huduma nzuri tunaomba serikali isikie kilio
chetu itusaidie” Alisema Fatuma.
Naye Bw,Emmanuel John alisema ubovu wa barabara hiyo
umechangia baadhi ya madereva wa piki piki kushindwa kufika hata
pindi wanapokuwa na wagonjwa hivyo kujikuta wakipata shida kubwa zaidi kutokana
na ubovu huo.
Hata hivyo Diwani wa kata hiyo,Michael Kapaya alikili kuwepo kwa
ubovu wa barabara hizo na kwamba kwa sasa bajeti za utengenezaji unafanywa na
TARURA na wamekwisha kuziingiza kwenye bajeti hivyo anatarajia muda wowote
zitaanza kujengwa.
Kaimu meneja wa Tarura halmashauri ya mji Bw ILDEPHONCE ZIRIRA
amesema ujenzi wa barabara unaenda kwa hatua kwa hatua na kwamba wamekwisha
pereka bajeti ya mwaka 2018 /19 hivyo anaamini mwaka huu zitajengwa
kwenye maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya uharibifu.
No comments:
Post a Comment