Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi na baadhi ya viongozi wakati wa shughuli ya uzinduzi wa magereza Wilayani Chato mkoani Geita. |
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba amemuagiza mkuu wa
jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro na timu ya uchunguzi kutoka jeshi la
polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina
Baftaha ambaye alikuwa ni mwanachuo wa chuo cha usafirishaji (NIT) yaliyotokea
wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam.
Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani Geita wilaya ya Chato
wakati wa uzinduzi wa gereza la wilaya ya Chato.
Waziri Dk. Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio
hilo na kujua hatua kwa askari aliyehusika na hilo na kuwaambia wananchi nini
kinachoendelea.
"Kama waziri mwenye dhamana nalaani vikali sana tukio la kupoteza
maisha ya binti wetu ambaye hakua na hatia, matukio ya namna hii naona yanaanza
kujirudia tena kwa kasi matukio ya kupoteza maisha kwa watu wasiokuwa na hatia
hasahsa katika maswala yanayohusu siasa ni mambo ambayo hayakubaliki na
ninalaani kwa nguvu zote",Alisema Waziri Mwigulu.
Ameongeza kusema kuwa amemuelekeza IGP mala baada ya tukio kutokea
wafatilie na wachunguze kubaini wote waliosababisha tukio la hilo na
kuweza kuwafikisha katika mkono sheria ili sheria ichukue mkondo wake.
Dk. Mwigulu amewataka wananchi wote kuepuka vitendo hivi vinavyoweza
kusababisha madhara kwa namna moja au nyingine na wanapoona matukio ya namna
hii watoe ushilikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili wausika wafikishwe
katika vyombo vya usalama.
No comments:
Post a Comment