Mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita juu ya kuendelea kuwatumia mafundi wa ngazi za mitaa (Local fundi) kwenye miradi ya jamii. |
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita ,Elisha Lupuga akizungumza na madiwani wakati wa kikao cha kawaida cha robo ya pili cha baraza hilo. |
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha kawaida cha robo ya pili cha baraza. |
Na Maduka Joel, Geita
Akizungumza wakati wa kikao cha kawaida cha robo ya pili cha baraza la
madiwani Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw Elisha Lupuga amewataka
Madiwani hao kuwatumikia wananchi kikamilifu na kuachana na mambo yanayoweza
kuzorotesha maendeleo.
“Kipindi hiki ni cha kufanya kazi na
kuwatumikia wananchi Utakiwi kuwa diwani wa kulalamika kwani ukuchaguliwa na
wananchi hili uwe kiongozi wa ambaye unakuwa na malalamiko bila ya kutafuta
njia ambazo zinaweza kusaidia kutatua changamoto za wananchi ambao unawaongoza
natambua Rais wetu kwasasa anasisitiza tufanye kazi za kuwatumikia wananchi
wetu” Alisisitiza Lupuga.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi
aliwataka madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Geita kufanya kazi
kwa ushirikiano kuhakikisha wilaya hiyo inapiga hatua na kuchochea maendeleo ya
wananchi.
Pia amesisitiza suala la kutumia mafundi wa ngazi za mitaa katika
kukamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule na afya ili kupunguza
gharama za wakandarasi ambao hutoza fedha nyingi.
Mhandisi Luhumbi pia amewakumbusha madiwani kuhoji miradi yote kwenye
kata zao na Halmashauri kwa ujumla ambayo inafadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa
Geita, GGM kwa madai kuwa baadhi ya miradi imekua na gharama kubwa kuliko
uhalisia wake.
No comments:
Post a Comment