Naibu waziri wa madini Stanslaus Nyongo
amewata wachimbaji wadogo wa mgodi wa Nyakafulu na Bingwa kudumisha
amani na utulivu katika shughuli zao ikiwemo kujenga
desturi ya kufanya usafi wa mazingira ili kuepukana na magojwa ya mlipuko
na iwapo hawatazingatia hayo migodi hiyo itafungwa.
Hayo aliyasema wakati wa ziara yake ya kuwatembelea
wachimbaji wadogo kwenye wilaya za Mbongwe na Geita.
Alisema ni vyema wachimbaji
hao kuzingatia amani na afya zao kwani ndio utaratibu uliowekwa na serikali
iwapo ikitokea magonjwa ya mlipuko
kama kipindupindu migodi hiyo itafungwa mara moja.
“Mpo hapa kwa sababu ya kauli ya
Mheshimiwa Dkt, John Magufuli lakini vilevile akisikia kwamba hapa hakuna amani
na sio wasafi mimi nitatoa amri ya kufunga mgodi huu kwani wizara
yangu ndio inahusika kutoa leseni hivyo pamoja na
hayo yote amani itawale” alisema Naibu waziri.
Kwa upande wake Rais wa shirikisho
la wachimbaji wadogo wa madini nchini Bw John
Bina aliwasisitiza wachimbaji wadogo kujenga desturi ya kulipa
kodi ili waweze kuchimba kwa kufata utaratibu, sheria, na kanuni za
nchi bila bugudhi yoyote na wagawane kwa utaratibu bila kudhulumiana
kwa sababu sehemu wanayochimba kuna leseni ya mtu kwa hiyo wachimbe kwa kuweka
akiba ili na wao baadae wakate leseni zao za uchimbaji.
‘Wachimbaji mmekuwa na tabia ya kula bata na kuhonga
pesa zote mnapouza madini acheni tabia hiyo wekeni akiba mkate
leseni zenu za uchimbaji zitawasaidia hapo baadae’ Alisema Bina.
Hata hivyo wachimbaji hao
wamemuomba Naibu waziri wa madini Nyongo kuwasaidia kupata leseni
ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yao na vitendea kazi kwa sababu wamekuwa
wakitumia njia za asili katika kufanya shughuli zao za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini,Staslaus Nyongo amemaliza
ziara yake ya siku tatu mkoani Geita,kwa kutembelea migodi mikubwa na midogo
huku akisikiliza kero za wachimbaji wadogo na kutatua changamoto ambazo
zilikuwa zikiyakabili maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment