Na Joel Maduka, Geita.
Waendesha Baiskeli Maarufu kwa jina la daladala wanaosafirisha abiria
kwenye halmashauri ya mji wa Geita, wamepinga agizo la Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo la kuwataka kufikia leo wasitishe shughuli zao kwenye maeneo
ya mjini badala yake wafanye kwenye maeneo waliyopangiwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya kupewa muda wa siku tano kupisha maeneo ya
mjini kutokana na wimbi la ajali zinazosababishwa na waendesha Baiskeli kwa
kutotumia barabara vizuri wanapokuwa kwenye shughuli zao.
Baadhi ya waendesha Baiskeli hao Bw Vistusi Maagani, John Maige na Fredy
Maganga wamesema utaratibu uliofanyika sio mzuri kwa kuwa hawajapewa maeneo
yatakayowasaidia kufanya kazi zao .
“Nasikitishwa sanaa na kitendo cha Mkurugenzi kututoa bila ya kutuandalia
maeneo mazuri ya kufanyia kazi zetu kwa mfano mimi hapa hii kazi ndio nategemea
kulisha familia pia kutuma pesa kwa mama yangu mzazi kwa kuwa sina ndugu leo
natolewa kufanya kazi mjini unategemea nitaishi maisha gani jamani na wale
ambao wananitegemea nitawaelezaje mimi naomba haya maamuzi wayaangalie kwa
umakini”Alisema Maagini.
“Nashindwa hata niseme nini najisikia moyo wangu kutoka kabisa
kutokana na taarifa hii ya kuondolewa mjini maeneo ambayo tunaambiwa kufanya
kazi akuna abiria sasa sijui tutaishije sisi waendesha daladala”Alisema
Maganga.
Bi,Lucia Paul ambaye mume wake anajishughulisha na kazi hizo
alisema kuondolewa mjini kwa waendasha baiskeli kutaleta athari kwenye
familia zao kutokana na wengi wao kutegemea shughuli hiyo kukidhi mahitaji ya
familia.
“Kwasasa hivi nyumbani hapakaliki kila siku
mume wangu anamawazo anashindwa afanye nini na uku anafamilia muda mwingine
hadi namuonea huruma serikali ni vyema ikaangalia maana itatupa wakati
mgumu sisi wanawake ambao tunawategemea waume zetu kwenye utafutaji” Alisisitiza Lucia.
Kutokana na hali hiyo chama cha ACT wazalendo kupitia kwa katibu wa mkoa
huo,Bw Ikolongo Otoo ameitaka halmashauri ya mji wa Geita kuondoa mara
moja zuio hilo kwa kuwa ni la kibaguzi ambalo alijazingatia wala
kuthamini vijana masikini na wanyonge ambao wameamua kujipatia vipato kwa njia
halali kabisa.
Mkurugenzi wa Halmashari ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly
alisema suala ambalo linafanyika ni la utekelezaji na alilikuwa aliitaji
muda kwani maeneo ambayo wamewapatia kufanya biashara ni makubwa na kwamba
hata wangepewa muda wa kutosha bado wangeombwa kuongezewa.
Mbunge wa Jimbo la Geita mjini,Constatine Kanyasu alisema
ahafikiani na makubaliano hayo na kwamba akuna utaratibu wala sheria
ambayo inawazuhia waendesha Baiskeli kufanya shughulo zao maeneo ya mjini.
No comments:
Post a Comment