Katibu tawala wa Mkoa wa Geita,Celestine Gesimba akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi. |
Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Mkoani humo. |
Na, Consolata Evarist Geita
Miongoni mwa Malengo hayo ni pamoja na yale yaliyoainishwa katika mpango
wa pili wa maendeleo ya miaka mitano pamoja na maendeleo endelevu.
Kata, Vijiji, Mitaa na vitongoji 34 mkoani humo vinatarajia kufanyiwa
utafiti huo ili kupata taarifa zinazohusu Kaya na wanakaya, Uzazi na
unyonyeshaji, elimu, afya, uraia, uhamiaji, ulemavu, bima, hali ya ajira,
biashara na mapato ya kaya na makazi ya kaya.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi alisema utafiti huo
utasaidia kuweka misingi katika kutambua viashiria vya kiuchumi, ajira na
ustawi wa jamii vitakavyofuatiliwa kwa kipindi husika na kupata makadirio ya
jumla ya mwenendo wa matumzi ya kaya ili kuandaa fahirisi za bei.
“Napende kuwahakikishia wananchi wa mkoa
wetu kuwa katika kutekeleza maagizo ya serikali ,uongozi wa mkoa umeendelea
kuhimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kutimiza azma ya
serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na yenye
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025” Alisema Luhumbi.
Amendelea kusema madhumuni ya utafiti huo wa mapato na matumizi ya kaya
binafsi Tanzania Bara wa mwaka 2017/18 ni kutoa takwimu za hali ya umasikini na
takwimu nyingine ili kusaidia serikali na wadau wengine kutathmini hatua
zilizofikiwa katika kutimiza malengo mbali mbali ya kitaifa na kimataifa
yakiwemo yale yaliyoanishwa katika mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa
miaka mitano (2016/17-2020/21) .
Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja
alisema azma ya serikali ni taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025
hivyo kutokana na misingi hiyo zinatakiwa ziwepo taarirfa sahihi kutoka kwa
wananchi.
Zoezi la utafiti ambalo linafanyika nchi nzima limeanza Desemba Mosi
mwaka jana na linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment