Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua kinu cha kuchakata dhahabu mara baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua baadhi ya mitambo ya uchenjuaji madini katika mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua njia ya kwenda kwenye mgodi wa chini mara baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Shanta uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza Wilayani Songwe, Leo 22 Februari 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesifu utendaji
unaofanywa na kampuni ya uchimbaji madini ya dhababu wa Shanta Gold Mine kwa
kukubali kuendana na matakwa ya serikali kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria
za nchi katika sekta hiyo.
Alisema kuwa Wizara hiyo imedhamiria kuboresha sekta ya Madini ili
wananchi waweze kunufaika na rasilimali hiyo ambayo imechezewa na wajanja
wachache katika kipindi cha muda mrefu.
Mhe Naibu Waziri huyo ametoa kauli hiyo Leo 22 Februari 2018 wakati
akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Shanta uliopo katika Kijiji na Kata ya
Saza Wilayani Songwe.
Kampuni ya SGM haipo kwenye kundi la wawekezaji walalamikaji kuwa
serikali kupitia sheria ya madini inawakimbiza wawekezaji jambo ambapo sio
kweli badala yake serikali imeweka utaratibu yakinifu wa uchumi fungamanishi
utakaoboresha sekta ya Madini na kuwanufaisha watanzania.
"Twendeni kwa watanzania tukawaulize wamenufaika kwa kiasi
gani na uwepo wa migodi mbalimbali ya uchimbaji nchini, jibu ni jepesi tu kuna
watu wachache wamenufaika na rasilimali hiyo jambo ambapo hatutalifumbia macho
tena" Alisema Mhe Biteko na kuongeza kuwa
"Serikali inahitaji wawekezaji ambao wanafuata sheria Na taratibu za
nchi hata kama ni wachache wanapaswa kufahamu kuwa wanapaswa kufuata sheria
kwani kufanya hivyo sio ombi bali ni lazima"
Aliongeza kuwa Wizara ya Madini itaendeleza ushirikiano kwa kiasi kikubwa
na mgodi huo ili kuinua zaidi uwekezaji wao na hatimaye kuwa na uzalishaji
wenye tija ambao utapelekea serikali kukusanya kodi kwa kiasi kikubwa kwa
manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla wake.
Alisema kuwa watumishi wote katika Wizara ya Madini na wawekezaji katika
sekta ya madini wanapaswa kusimamia haki katika utendaji wao huku wakiunga
mkono juhudi za serikali katika kuimarisha nidhamu ya uwajibikaji hususani
kujitenga na utoaji ama upokeaji wa rushwa.
Alisema dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kuwarahisishia huduma
wachimbaji wadogo kupitia malezi bora ya Wizara ya madini ili kufikia hatua ya
kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kufikia uwekezaji mkubwa katika uchimbaji
wa rasilimali hiyo.
Katika hatua nyingine wawekezaji hao wametakiwa kuwaamini wataalamu wa
Madini wa hapa nchini pasina kuwa na Mashaka nao kwani serikali inawafahamu na
wengi wao wakiwa wanafanya kazi nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment