Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018.
Picha ya pamoja Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (katikati) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla mara baada ya mazungumzo wakati alipozuru ofisini kwake akiwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, Leo 20 Februari 2018. Wengine pichani ni Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njenza CCM (Kulia), Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi Mariamu Mtunguja (Wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika (Wa kwanza kushoto).
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akisikiliza kwa makini taafifa kuhusu sekta ya madini kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto
Mashaka Biteko ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya ambapo pamoja na
mambo mengine atatembelea kiwanda cha kutengeneza Samani mbalimbali
zinazotokana na Marble, kukagua shughuli za uchakataji Madini ya malumalu na
mradi wa Pandahili (Niobiaum).
Maeneo mengine atakayotembelea ni
pamoja na mgodi wa Sunshine uliopo katika Wilaya ya Chunya ambapo atazungumza
pia na wachimbaji wadogo katika migodi atakayotembelea.
Mara baada ya kuwasili katika Mkoa wa
Mbeya Mhe Biteko amesifu juhudi za Mkuu wa Mkoa huo Mhe Amos Makalla kwa
uthubutu mkubwa katika utendaji ikiwa ni pamoja na usimamizi madhubuti katika
sekta ya Madini.
Pamoja na pongezi hizo Mhe Biteko
amemsihi Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya kuongeza juhudi zaidi ili kutimiza ndoto ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
kuwatumikia watanzania na kupelekea kunufaika na rasilimali zao ikiwemo sekta
ya Madini.
Alisema kuwa Sekta ya Madini bado ni
muhimu hivyo inahitaji kulelewa ili ikuwe na hatimaye kuongeza ufanisi katika
uchangiaji wa pato la Taifa
Alisema kila kiongozi ana wajibu
mkubwa kuwa mbunifu katika uwajibikaji wake huku akiongeza kuwa Jukumu la
msingi la kiongozi ni pamoja na kutafsiri ndoto za Rais Magufuli ili kuwafanya
wananchi kunufaika na uongozi bora na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mhe Amos Makala amesisitiza kuendeleza ushirikiano madhubuti na Wizara ya
Madini ili wananchi Mkoani humo wanufaike na matunda ya kukichagua Chama Cha
Mapinduzi kuongoza dola.
No comments:
Post a Comment