Katibu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw.
Godfrey Mngereza (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kujadili
mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya biashara wa
bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la
Sanaa za Ufundi Bw. Adrian Nyangamalle
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na wasanii wa sanaa ya uchongaji
pamoja na wafanya biashara wa kazi za uchongaji (hawapo pichani) wakati wa
kikao cha kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na
wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw. Adrian Nyangamalle
Mwenyekiti mstaafu Chama cha Wasanii Wachongaji
Tanzania (CHAWASAWATA) Bw. Focus Senya (kushoto) akitoa ufafanuzi wa mgogoro wa
umiliki wa ardhi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa kikao kujadili mgogoro wa umiliki
wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji
leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania
(CHAWASAWATA) Bw. Isihaka Abdul akielezea historia ya umiliki wa ardhi kwa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(hayupo pichani) wakati wa kikao kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge
kati ya wachongaji na wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es
Salaam.
Mmoja wa wajumbe wa chama cha Makonde Hand Craft
Village Bw. Hamis Mhando (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)
kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya
biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wanaojishughulisha na sanaa ya
uchongaji katika eneo la Mwenge wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa kikao cha
kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya
biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa tasnia ya
sanaa ya uchongaji haiwezi kuendelea kama mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge
utaendelea kuchukua nafasi kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila
siku hivyo kushindwa kujiinua kiuchumi na hata kushindwa kuchangia katika pato
la taifa.
Waziri Mwakyembe
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na wasanii wachongaji
pamoja na wafanyabiasha wa kazi za sanaa ya uchongaji kujadili mgogoro wa
umiliki wa eneo la Mwenge ili kuweza kuweka mikakati ya kutatua changamoto hiyo
iliyodumu kwa zaidi ya miaka 10.
Waziri Mwakyembe
amesema kuwa eneo la Mwenge lenye mgogoro lina uwezo mkubwa chini ya serikali
ya awamu ya tano kupata pesa nzuri kutoka kwa wawekezaji na kubadilisha muonekano
wake kutokana na eneo hilo kuwa na bidhaa nzuri zinazobuniwa na wasanii
wachongaji hivo kuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka mataifa mbalimbali.
“Tutarudi tena hapa
kuja kutoa msimamo wa serikali ni upi ili tuweze kuendelea, hii ni serikali ya
awamu ya tano haki lazima itendeke hiki sio kipindi cha wajanja wajanja
kuchezea haki za wenzao” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe
amewataka wasinii wachongaji pamoja na
wafanyabiashara wa kazi za sanaa ya uchongaji kuwa na umiliki wa pamoja na kutambuana
kama watoto wa baba mmoja na mama mmoja ili kuweza kuiendeleza tasnia hiyo ya
uchongaji kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu
Baraza la Sanaa la Taifa Bw. Godfrey Mngereza amesema kuwa lengo la kujadili
sintofahamu ya eneo la Mwenge ni pamoja
na kurekebisha sintofahamu hiyo ili wasanii wachongaji pamoja na wafanyabiasha
waweze kwenda kwa pamoja katika kujenga nchi hii kwani sanaa ni kazi, sanaa ni
uchumi lakini pia sanaa inazalisha ajira.
Naye Rais wa Shirikisho
la Sanaa za Ufundi Bw. Adrian Nyangamalle amesema kuwa nia kubwa ya shirikisho hilo
ni kuifanya tasnia ya sanaa za ufundi kufika mahala ambapo italeta mchango
unaokusudiwa kwa taifa na kubadilisha maisha ya wasanii na wadau wote wa tasnia
hiyo na hili hayo yafikiwe ni lazima kuwe na amani ili kila mtu awe na uhuru wa
kufanya kazi zake kwa nafasi.
Aidha Bw. Nyangamalle
amesema kuwa Shirikisho la Sanaa za Ufundi limeweza kupokea changamoto ya
umiliki wa ardhi hiyo na kuwasilisha kwa wadau na serikali kwa ajili ya
kusaidia kutatua changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment