Barabara ya kutua ndege (run away) yenye urefu wa Mita 300 ambayo kwa sasa hipo kwenye hatua nzuri za mwisho kukamilika. |
Baadhi ya watendaji na wajumbe wa Bodi ya TANAPA wakikagua ujenzi wa mradi wa uwanja wa Ndege Wilayani Chato Mkoani Geita. |
Kukamilika kwa ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wilayani
Chato mkoani Geita unatarajia kuwavutia watalii wengi kutembelea kivutio
cha hifadhi ya Taifa cha Rubondo Kilichopo mkoani humo .
Ujenzi wa uwanja huo umeanza rasmi mwezi wa Septemba mwaka
jana na unatarajia kukamilika Juni mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa bodi ya
wadhamini (TANAPA), Jenerali Mstaafu
George Waitara wakati alipotembelea uwanja huo
pamoja na wajumbe wa bodi hiyo na baadhi ya
watendaji kwa nia ya kujionea maendeleo ya
ujenzi huo ambao umeelezwa
kukamilika kwa asilimia 65.
“ Kiukweli niseme kazi kubwa sana ambayo
imefanyika ya ujenzi wa uwanja huu utakuwa na faida kubwa sana kwaajili
ya mambo ya utalii na mambo mengine kama ya biashara na suala jingine kubwa ni
kuibua vivutio vingine tupate watalii wengi zaidi , tunatarajia
utakapokamilika utaleta manufaa sana katika sekta
mbali mbali zikiwemo za utalii na biashara
mkoani Geita na mikoa ya jirani,” Alisema Waitara.
Kwa upande wake, Mhandisi wa ujenzi
wa uwanja huo,Makuye Muhinga,Alisema uwanja huo wenye
barabara ya kutua ndege (run a way )
yenye urefu wa Mita 300 upo kwenye hatua nzuri
na kwamba wanatarajia kukamilisha mwaka huu ujenzi wa
uwanja.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa huo , Mhandisi Robert Gabriel
Luhumbi ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu ambao wametembelea
uwanja huo alisema kukamilika kwa uwanja huo kutafungua uwigo mpana wa kiuchumi
kutokana na kwamba mkoa utaweza kutembelewa na wageni kutoka mataifa ya nje na
jirani.
“Wito wangu kwa wananchi ni kuhakikisha wanachangamkia
fursa mbalimbali za maendeleo hasa
uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kuchakata
mazao yalimwayo mkoani humu, na tunaamini uwanja
huu utarahisisha usafirishaji wa bishara ambazo
watakuwa wanazifanya badala ya kupitia Mwanza sasa hivi wataweza kupitia kwenye
mkoa wao”Alisema Luhumbi.
Jumla ya hifadhi zilizopo nchini ni 16 ambazo zinatambulika kimataifa
ikiwemo na hifadhi ya Rubondo ambayo hipo Mkoani Geita.
No comments:
Post a Comment