Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa amezitaka
halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila kijiji kinakuwa na shule ya
msingi yenye madarasa ya awali na kila tarafa iwe na shule ya kidato cha tano
na cha sita.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo jana Wilayani
Sengerema Mkoani Mwanza katika ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza ambapo
amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango bali wajikite na
taaluma.
Waziri Mkuu Majaliwa katika siku yake ya kwanza mkoani humo
akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alizindua madarasa manne ya
kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Nyehunge wilayani sengerema
huko na kutoa maagizo hayo.
No comments:
Post a Comment