Tuesday 21 March 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MPANGO WA USAJILI NA UTOAJI WA VYETI VYA KUZALIWA KWENYE MIKOA YA GEITA NA SHINYANGA

Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe  akizindua Mpango wa Usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri wa miaka  Mitano kwenye mikoa ya Geita na Shinyanga.

Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe akionesha simu janja ambayo itatumika kwenye zoezi hilo.








Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe  amezindua Mpango wa Usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri wa miaka  Mitano kwenye mikoa ya Geita na Shinyanga.

Uzinduzi huo ambao umefanyika kwenye viwanja vya kalangalala mjini Geita,umehudhuriwa na wakuu wa Mikoa yote Miwli  pamoja na viongozi wa wakuu wakiwemo wakuu wa wilaya,wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote,makatibu tawala wa mikoa na wilaya,waganga wakuu wa mikoa hiyo,waganga wakuu wengine wa idara na wananchi mjini Hapa.

Akito Takwimu za sense ya watu na makazi ya mwaka 2012  Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya wakala wa usajili,ufilisi na udhamini(RITA) Bi,Victoria Lembeli,amesema kuwa  ni asilimia kumi na tatu pointi nne ya wananchi wa Tanzania Bara ndio ambao wamesajiliwa na kupatiwa vyeti hali ambayo sio nzuri kwa Taifa.

Kwa upande wa UNICEF, Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania Rene Van Dongen alisema “ Kila mtoto ana haki ya kutambuliwa  na Cheti cha kuzaliwa ni taarifa muhimu ya awali inayothibitisha kuzaliwa kwa mtoto,Kwa sasa Tanzania ina kiwango cha chini sana cha usajili wa watoto, hali inayoashiria idadi kubwa ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano hawatambuliki katika taarifa za serikali , Mpango huu utaongeza kasi ya usajili wa watoto na fursa ya kupata haki yao ya msingi na kwa upande wa serikali itakuwa na taarifa sahihi kwa ajili ya mipango na sera”Alisema Dongen.

Serikali ya kanada ambayo ni mfadhili wa mpango huu inatambua haki za watoto na ina amini kila mtoto anahitaji utambulisho wa kudumu wa kuzaliwa unaotambulika na nchi kisheria na ni haki ya msingi ya mtoto.  Ufadhili umechangia juhudi za serikaliza kuboresha mpango wa kuduma wavyeti vya kuzaliwa unaoenga kufikia watoto million tatu na nusu (3.5 million) walio.

Akiwahutubia wananchi mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo ambaye ni  Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe,amewaasa watanzania Kujenga utamaduni wa kusajili kila mtoto anayezaliwa ili aweze kutambuliwa ndani na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake ikiwa ni pamoja  na kutoa taarifa za kila mtu anayefariki .

Baadhi ya wananchi ambao wamezungumza na Storm Habari Mkoani Hapa, Ivon Mashaka  na Abubakari Magembe wamesema kuwa wanaishukuru serikali kwani imerahisisha kwa wananchi wasiyokuwa na uwezo kupata vyeti bila ya gharama yoyote.


Mpango wa usajili wa  wa vizazi na vifo utasaidia kuziba pengo la mgawanyo uliopo kati ya mijini na vijijini kwa kupeleka huduma za usajili kwa watoto walio chini ya umri wa Miaka mitano kwa jamii zilizoko pembezoni.



No comments:

Post a Comment