Tuesday, 21 March 2017

TAZAMA PICHA MBALI MBALI ZA TUKIO LA UZINDUZI WA MPANGO WA USAJILI NA UTOAJI VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO WAUMRI CHINI YA MIAKA MITANO KATIKA MIKOA YA GEITA NA SHINYANGA

Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe  akizindua Mpango wa Usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri wa miaka  Mitano kwenye mikoa ya Geita na Shinyanga.


Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe,akiwasili kwenye viwanja vya kalangalala ambapo ndio zoezi la uzinduzi lilikuwa likifanyika.




Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Geita na Shinyanga.


Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.huku akiongozana na mwenyeji wake ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi.


Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe,akisalimiana na viongozi wa Dini Mkoani Geita.





Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe,akisalimiana na Meneja wa Kanda ya Ziwa wa TIGOAlly Maswanya.


Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe,akifuatilia burudani ambazo zilikuwa zikiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu,pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matito wakifuatilia  shughuli ya uzinduzi.

Katibu wa vijana  chama cha mapinduzi wilaya ya Geita  ambaye ndiye alikuwa ni mshehereshaji wa shughuli hiyo Ally Rajabu akitoa maelekezo kwa wananchi.

Zoezi la uhandikishaji likiendelea kwenye viwanja vya kalangalala Mkoani Geita,



Baadhi y wakina mama na watoto wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kujiandikisha.

Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale  Hamim Gwiyama na Mkuu wa wilaya ya Geita wakiingia kwenye viwanja vya kalangalala.

Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale  Hamim Gwiyama akipiga hatua kuelekea jukwaa kuu.

Kwaya ya A.I.C Kalangalangalala wakiimba wimbo wa kuhimiza wazazi kujitokeza kuwaandikisha watoto wao vyeti vya kuzaliwa.



Mbunge wa Geita Vijijini  na mwenyekiti wa CCM Mkoani Geita Joseph Kasheku Msukuma akielezea  RITA Kuwashirisha wazawa kwenye zoezi hilo ili kuepuka baadhi ya watu ambao sio raia wa Tanzania kujisajili  ili kupata vyeti vya kuzaliwa.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi,Zainabu Teleck akitoa neno wakati wa uzinduzi.

Wakuu wa Mikoa ya Geita na Shinyanga wakiongozwa na Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe Wakitazama burudani ya Ng'oma.

Kaimu afisa mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson akielezea dhamira na malengo ya mpango wa kutoa vyeti kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Mwakilishi wa serikali ya Canada Bi,Suzan Stephania akielezea namna ambavyo Serikali ya Canada ambayo ni mfadhili wa mpango huu inavyotambua haki za watoto na ina amini kila mtoto anahitaji utambulisho wa kudumu wa kuzaliwa unaotambulika na nchi kisheria na ni haki ya msingi ya mtoto. 

Meneja wa Kanda ya Ziwa wa TIGOAlly Maswanya, alifafanua kuwa  “Ushiriki wa TIGO uko katika mpango wa kuboresha matumizi ya digital katika maisha kwa kushirikiana na UNICEFna RITA kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa anapata fursa ya kuandikishwa


Burudani ni sehemu ya maisha hapa ni Mcheza Ng'oma za asili akiendelea kufanya yake .


Waziri Mwakyembe akiwatunza vijana waacheza Ng'oma.


Afisa Mtendaji wa kata ya Kalangalala akitoa maelezo juu ya Namna zoezi la usajili linavyoendelea.

Baadhi ya wafanyakazi wa UNICEF Wakiwa kwenye picha ya pamoja na waziri Mwakyembe.

Akiwahutubia wananchi mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo ambaye ni  Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe,amewaasa watzaniaan Kujenga utamaduni wa kusajili kila mtoto anayezaliwa ili aweze kutambuliwa ndani na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake ikiwa ni pamoja  na kutoa taarifa za kila mtu anayefariki .

Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe akitoa vyeti kwa watoto watano.

Mh,Msukuma na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakiteta jambo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akisisitiza umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa wakati wa uzinduzi.




No comments:

Post a Comment