Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu
za pole kutoka Serikalini katika tukio la kuaga mwili wa
aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya
Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu
Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12
Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
tukio hilo limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw.Abdurahaman Kinana akitoa salamu
za rambirambi za Chama wakati
wa kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania na Chama Cha
Mapinduzi katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement
Jaji Mstaafu Mhe.Joseph Sinde Warioba akitoa salamu za pole wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa
kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa
mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama
Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa
salamu za pole katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa
Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George
Clement Kahama
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa heshima za mwisho
kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania
katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama
Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Jamhuri ya
Muunganowa Tanzania Mhe. Alhaji Ally Hassan
MwinyiakitoaheshimazamwishokwamwiliwaaliyekuwakiongoziwaSerikali ya
Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu
Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Makamu wa Rais mstaafu katika Serikali ya awamu ya
Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa
kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa
mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili
Mjane wa Marehemu Sir. George Clement Kahama Mama Janet Kahama (wa
pili kushoto) akiwa na familia yake wakati
wa Tukio la kumuaga mume wake ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Serikali
ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali aliyefariki tarehe
12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa
Serikali imesema itaendelea
kuenzi na kuheshimu mchango mkubwa katika kupigania maendeleo na ustawi wa jamii
uliofanywa na marehemu Sir George Kahama
enzi za uhai wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya
Tanzania.
Hayo yamesemwa leo Jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
alipokuwa akitoa salamu za Serikali katika tukio la kumuaga mmoja wa waasisi wa
Taifa na Waziri msataafu marehemu Sir
Gorge Kahama aliyefariki dunia Machi 12 mwaka huu katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili.
Waziri Nape amesema kuwa Sir George Kahama alikuwa kiongozi mahiri na aliyetekeleza
majukumu yake kwa ufasaha ambapo alikuwa miongoni mwa viongozi walioanzisha harakati
za Serikali za uendelezaji wa mji wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuimarisha makao makuu ya nchi.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdurahaman Kinana amemueleza
Sir George Kahama kama kiongozi mahiri katika Chama
aliyependa maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla katika weledi wa hali ya
juu na alikuwa mchapakazi.
Marehemu Sir
George Kahama amekuwa Waziri na
Kiongozi kabla na Baada ya Uhuru wa
Tanzania Bara kuanzia awamu ya kwanza hadi
ya tatu ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambapo amezikwa leoJijini
Dar es Salaam na ameacha Mjane na Watoto.
No comments:
Post a Comment