Jumla ya Nyumba 40 kwenye kata ya
Buhala hala Wilayani Geita zimeezuliwa na zingine kubomoka kutokana na mvua
iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi hali ambayo imesababisha baadhi ya wananchi
kukoswa makazi.
Dafroza Kadike ni moja kati ya wananchi wa mtaa wa Mwatulole ameelezea
kuwa siku hiyo majira ya saa moja usiku mvua kubwa ikiambatana na radi
ilinyesha na kusababisha nyumba nyingi kuezuliwa na zingine kuanguka kutokana
na upepo .
Aidha kwa upande wake John Slvesta,ameiomba serikali katika wilaya ya
Geita kutoa msaada kwa watu ambao wameathirika kwani wananchi wengi kwasasa
wapo nje kutokana na makazi yao kuharibiwa.
Diwani wa kata hiyo,Mussa Kabese amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kwamba
amewataka wananchi kuwa na subira kwani hataakikisha anafikisha kwenye kamati
ya maafa iliyopo Mkoani Geita.
“Mimi Nikiwa kama kiongozi wa kata hii ya Buhala hala nimesikitishwa na
kile ambacho kimetokea kwa wananchi kuharibiwa makazi yao kutokana na mvua
iliyo nyesha niwaombe tu wananchi ambao wamepatwa na maafa haya kujiandikisha
kwa watendaji”alisema Kabese.
|
No comments:
Post a Comment