Baadhi ya
akina mama wanao fanya biashara katika soko linalo milikiwa na chama cha
mapinduzi (CCM) katika mamlaka ya mji
mdogo wa katoro wilayani na mkoani Geita wamelalamikia uongozi wa eneo hilo kwa
kuwavunjia meza zao za biashara kwa madai ya kuto lipa kodi .
Tukio hilo limetokea march 18, 2017 ambapo jumla ya
meza nne zimeondolewa katika soko hilo kwasababu zinazo elezeka kuwa kina mama
hao wameshindwa kulipa pango la ardhi katika soko hilo.
wakizungumza kina mama hao ambao wanatambulika kwa
majina ya Agnes Gervas, Pendo Kayanda, Agnes Juma na Lusia Lukas wamesema kuwa
utaratibu wa kulipa kodi katika eneo hilo huwa wanalipa kila ifikapo tarehe 20
ya mwezi wa 4 lakini imekuwa tofauti kwa mwaka huu ambapo wametakiwa kulipia
meza hizo mwezi wa tatu mwaka huu.
Aidha wameiomba Serikali kuwatengea eneo la kufanyia
shughuli zao za kibiashara kutokana na kunyanyaswa katika soko hilo
Kwa upande wake msemaji wa kamati ya soko hilo Rashid
Shaka amesema kuwa utaratibu wa ukusanyaji kodi umebadilika na taarifa za
mabadiliko hayo zilifikishwa kwa wafanya biashara wote kabla ya
utekelezaji wa ukusanyiaji mapato
kuanza.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Katoro Philimoni Mgoyezi ameeleza kuwa taarifa za
kuondolewa kina mama hao amezipata na ameiomba kamati husika kutotumia nguvu
kubwa kwa wafanyabiashara katika soko hilo na badala yake watumie busara wakati
wa kutatua migogoro inayo jitokeza.
No comments:
Post a Comment