|
Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,akizungumza wakati wa kikao cha tasmini juu ya maeneo na migodi ambayo wamezungukia Mkoani Geita. |
|
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mara Joyce Sokombi akiandika baadhi ya point zilizokuwa zikizungumzwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo. |
|
Wajumbe wakifuatilia Kikao. |
|
Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,akitoa maagizo kwa wanufaika wa Ruzuku. |
|
Kaimu Kamishna wa Madini ,Mhandisi Ally Samaje akimwakikishia
Mwenyekiti wa kamati hiyo kutekeleza maagizo ambayo ameyatoa. |
|
Naibu Katibu Mkuu Prof,James Mdoe,akisisitiza kwa wachimbaji ambao wamepatiwa
Ruzuku mpango wa kuwazungukia wote. |
|
Mwenyekiti wa halamshauri ya Mji wa Geita,Lernad Kiganga Bugomola akijitambulisha kwa wajumbe. |
|
Meneja Mahusiano ya jamii mgodi wa GGM ,Manase Ndoloma akielezea namna mgodi huo umekuwa ukichochea maendeleo kwa wananchi Mkoani Geita. |
Kamati
ya Bunge ya Nishati na Madini imeitaka
wizara hiyo na Stamico kuangalia ubia na leseni ya mgodi wa Buckreef Gold Company Limited uliopo Rwamgasa ambao kwa muda umekuwa ufanyi kazi
za uchimbaji huku kuna wachimbaji wadogo wamekuwa wakihitaji
kufanya shughuli za uchimbaji kwenye
maeneo ambayo yameshikiliwa na mwekezaji .
Akizungumza
baada ya ziara ya siku nne Mkoani Geita,Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,amesikitishwa na mwekezaji wa Backreef
kushikilia eneo kubwa huku kuna baadhi ya wananchi wanaidai kampuni hiyo fedha
nyingi.
“Kuna eneo
la Backreef tunakuomba sana na tunaitaka
Wizara na Stamico muende mfanye haraka sana muangalie patna ship zenu mnaleta wabia ambao kwa sehemu kubwa ni
wajanja wajanja tu hakuna wanachofanya eneo wamelikalia wachimbaji wadogo wadogo mngewapatia eneo
hilo ingekuwa na maana kubwa zaidi kuliko mnampatia mtu mmoja mgeni anashika
eneo kubwa leseni 13 kwa miaka yote hakuna anacho fanya halafu tunaona sisi
watanzania tumezidiwa akili na mtu mmoja hilo halikubaliki lakini msimamie kuna
madeni ambayo watanzania wanamdai ahakikishe anayalipa”Alisema Biteko.
Sanjari na
hayo Mwenyekiti Biteko,ameitaka wizara kuhakikisha fedha za ruzuku zinawafikia
walengwa na kwamba pesa hizo zisipelekwe kwenye matumizi ambayo ni kinyume na
shughuliza za uchimbaji.
Hata hivyo
kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Madini
,Mhandisi Ally Samaje amemwakikishia Mwenyekiti wa kamati hiyo kutekeleza
maagizo ya kamati ikiwa ni pamoja na fedha za ruzuku kufanya kazi ambazo zinatakiwa.
Naibu Katibu
Mkuu Prof,James Mdoe,amesisitiza kuwa kwa wachimbaji ambao wamepatiwa Ruzuku kuna mpango wa
kuwazungukia wote na kujua namna ambavyo wametumia fedha hizo na kwamba hoja
zote zilizozungumza watazijibu kwa maandishi kujua maamuzi ambayo wameyachukua
kutokana na fedha za ruzuku.
No comments:
Post a Comment