Thursday 2 March 2017

MRADI MKUBWA WA MAJI KUMALIZA KERO YA MAJI HALMASHAURI YA MJI WA GEITA

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Geita,Constatine Kanyasu wenye lengo la kutatua na kusikiliza Kero za wananchi.

Diwani wa Kata ya Nyankumbu Wilayni Geita,Michael Kapaya akielezea  namna ambavyo amejipanga kutatua kero za wananchi ambao anawaongoza

Mbunge wa Geita Mjini,Constatine Kanyasu,akijibu baadhi ya changamoto na Kero ,ambazo zimeulizwa na wananchi.

Moja kati ya wananchi wa Kata ya Nyankumbu Mzee,Lukas Ngwesaga,akielezea namna ambavyo wazee wamekuwa wakikutana na shida kwenye huduma ya afya.

Bi,Lemmy Masalu akimwomba Mbunge kuwasaidia  fedha za TASAF  kuongezewa.


Meneja ufundi wa Gewasa,Isaac Mgeni Akijibu juu ya kero ya maji.
Mbunge wa Geita Mjini akisikiliza kwa makini Mkutano.




Huduma ya maji katika mji wa Geita  Bado ni tatizo  kubwa kwani watu ambao wanapata maji safi na salama kwa sasa ni Asilimi 36  huku lengo la serikali ni kuhakikisha asilimia 90 wanapatiwa huduma ya maji katika miji.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika kata ya Nyankumbu mmoja kati ya wananchi, Bi,Angelina Richard  amemwambia mbunge  wa Geita Mjini ,Constatine Kanyasu kuwa tatizo la maji limekuwa ni tatizo kubwa hususani kwa wakina mama hali ambayo imekuwa ikitishia kuvunjika kwa miji yao.

“Mheshimiwa Mbunge kiukweli sisi wakina mama tumekuwa tukiingia kwenye malumbano na familia zetu sababu kubwa ni kutokupatikana kwa maji tunakuomba kama mwakilishi wetu utusaidie”Alisema Bi Angelina.

Kutokana na Ombi hilo ,Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu,alisema kuwa wamepata Bilioni mia moja kutoka serikali ya India ambazo zimekopwa na serikali ili kusaidia upatikanaji wa maji katika maeneo ambayo yamekuwa na changamoto.

“Mkandarasi anatarajia kuanza kazi mwezi wa saba kwa kuakikisha anasambaza maji kwenye maeneo ambayo yameonekana kuwa na changamoto kubwa ya maji kwenye halmashauri ya mji wa Geita kwa hiyo niwahakikishie wananchi kuwa swala hili tunashughulika nalo na tutaakikisha changamoto hii tunaimaliza”Alisema Kanyasu

Aidha kwenye mkutano huo,meneja ufundi wa Gewasa,Isaac Mgeni ,akisema  kuwa tatizo la kukatika kwa maji linatokana na matengenezo ya miundo mbinu ambayo imekuwa ikitumika  kutibia maji pamoja na kukatika kwa umeme  kuwa kwenye matengenezo lakini hata hivyo bado wapo kwenye jitihada za kukomesha kero hiyo.

Diwani wa Kata ya Nyankumbu Michael Kapaya amewataka wananchi  hao kuwa na subira kwani serikali imejipanga kutatua changamoto zinazo wazunguka hususani za miundo mbinu.

IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE

No comments:

Post a Comment