Friday 24 March 2017

WATAALAMU WA LUGHA WAOMBWA KUTAFSIRI FILAMU ZA KISWAHILI KWA LUGHA YA KICHINA ILI ZIPATE SOKO NCHINI CHINA



Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na hadhira (haipo katika  picha) katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG GANG (wa kwanza kulia) kabla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi vya Luninga  Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi Suzan Mungy akizungumza na hadhira (haipo katika picha) akitoa maelezo mafupi kuhusu Shirika hilo linavyoshirikiana na Serikali ya China  katika  hafla ya  Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya ya kichina inayoitwa  “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Naibu Waziri wa Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG GANG wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya ya kichina inayoitwa  “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika

 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Naibu  wa Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG GANG (katikati waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandaaji na washiriki wa  Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba Wataalamu wa lugha ya Kichina hapa nchini kutafsiri Filamu za Kiswahili kwa lugha ya kichina ili zipate soko nchini China.

Prof. Elisante Ole Gabriel ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazindua Maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya kichina  inayoitwa “Mfalme Kima” iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo amesema kuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa watanzania katika filamu za kichina ni kutumia lugha ya Kiswahili.

“Njia rahisi ya kufikisha ujumbe  kwa watu wote ni kutumia lugha mtambuka katika tamthiliya  zetu hii itasaidia sana kukuza uhusiano wetu na Jamhuri ya Watu wa China”,Alisema Prof.Ole Gabriel.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi vya Luninga Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi Suzan Mungy ameelza kuwa ushirikiano wa shirika hilo na Kampuni ya Star Times ambayo ndio waandaji wa Tamthiliya hiyo umeleta mafanikio makubwa ikiwemo  kuongezeka kwa watazamaji wanaopenda tamthiliya za kichina zenye tafsiri ya lugha ya Kiswahili zinazooneshwa katika luninga hiyo.

“Ushirikiano wetu unazidi kuimarika na tunaamini utaleta mafanikio makubwa zaidi kwetu sote katika kutoa elimu na Burudani kupitia Tamthiliya na vipindi vingine  vinavyopatikana katika visimbuzi vya Star Times”,Alisema Bibi Suzan.


Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya Kichina “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili imezinduliwa leo Jijini Dar es Salaam ambapo maudhui yake yanatoa elimu pamoja na Burudani.

No comments:

Post a Comment