Thursday 16 March 2017

WAZIRI NAPE - MAPITIO YA MKATABA KATI YA TBC NA STRATIMES KUMALIZIKA MWEZI APRIL





Waziri wa Habari Utamaduni  Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyesimama) akizungumza na Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Jamii pamoja na Uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati kamati hiyo chini ya mwenyekiti Mhe. Peter Serukamaba (Mb) ilipotembelea Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Kamati  ya  Bunge ya maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba (Mb) (aliyesimama) akitoa maelezo mafupi kuhusu dhumuni  la  ziara ya kamati hiyo katika  Shirika la Utangazaji  la Taifa (TBC) katika kikao kazi wakati kamati hiyo  ilipotembelea TBC  leo Jijini  Dar es Salaam .Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni  Sanaa  na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.



Mkurugenzi  wa Shirika la laUtangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Ryioba (aliyesimama) akieleza utendaji kazi wa Shirika kwa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Jamii wakati kamati hiyo ilipotembelea TBC leo Jijini Dar esSalaam. Kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni  Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Mbunge wa Jimbo  la Ilala Mhe. Mussa Zungu.


No comments:

Post a Comment