Tuesday, 28 March 2017

HALMASHAURI YA MJI YAKABIDHI VYOO VYA KISASA KWENYE SHULE ZA MSINGI .

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali akizindua vyoo vya kisasa vya wanafunzi wa shule ya Msingi Mbugani.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali  akiongozana na mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mbugani kwenda kukagua vyoo hivyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali ,akikagua vyoo vya shule ya msingi Mbugani.


Sehemu ya kunawa mikono pindi wanafunzi wanapotoka msalani.

Muonekano wa choo cha kisasa cha kufrashi.

Choo cha watu wenye ulemavu.

Walimu pamoja na wanafunzi wakifatilia kwa makini maelekezo ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinali  akisisitiza jambo kwa walimu na wanafunzi kuvitunza vyoo hivyo.




Halmashauri ya Mji wa Geita,imekabidhi vyoo vya kisasa kwa shule za msingi za Nyankumbu,Kivukoni pamoja na Mbugani ambao umegharimu kiasi cha sh,million mia moja na ishirini.

Akielezea namna ya mradi huo ulivyoanza na kumalizika Mhandisi wa shirika lililokuwa likisimamia Mradi huo la Acoil Godfey Wandi amesema kuwa mradi huo umefadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika na ujenzi ulianza mwaka 2015 na 2016 ulikamilika na kwamba ni vyoo vya kisasa kwani kuna sehemu za watu wenye ulemavu.

“Kwa sasa hivi mradi umekamilika na upo tayari kwa ajili ya matumizi kuna majengo mawili jengo la wasichana na jengo la wavulana na bila shaka leo wanafunzi wanaweza kuanza kutumia vyoo hivi”Alisema Wandi.

Kwa upande wake Kaimu afisa elimu halmashauri ya Mji wa Geita,Mwl Salome Cherehani  ameishukuru Benki ya maendeleo ya afrika na kwamba wanaamini kukamilika kwa ujenzi huo utapunguza kero na  adha ambazo zimekuwa zikijitokeza kutokana na upungufu wa vyoo.

Mkuu wa shule ya msingi Mbugani Forenci Lernad ,amemweleza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwa kutokana na hali ilivyokuwa choo cha shule kilititia na kusababisha idadi ya matundu ya choo kupungua shuleni hapo.

Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Mhandisi Modest Aporinali amewataka walimu pamoja na wanafunzi kuhakikisha wanavitunza vyoo hivyo ili viweze kudumu.

No comments:

Post a Comment