Serikali mkoani geita
imewataka wananchi kuwafichua watu wanajihusisha na vitendo vya ukatili kwa
watoto wadogo waishiyo katika mazingira magumu
kwani kwa kufanya hivyo nikuwasaidia watoto kutoka katika wimbi hilo ambalo limekuwa
likiwapatia wakati mgumu.
Hatua hiyo imekuja mara
baada ya mtoto mdogo anaekadiliwa kuwa na umri wa kuanzia miaka kumi ambaye anatambulika kwa jina la Nestori Safari
mkazi katika mamlaka ya mji mdogo wa
katoro amejikuta katika wakati mgumu ambapo ndugu aliye kuwa akiishi nae
kamfanyia ukatili wa kinyama.
Akizungumza mtoto huyo
amesema kuwa kitendo hicho alifanyiwa na jirani yake ambae alikuwa akiishi nae
ambapo alimfunga manati kwenye mikono yake miwili kisha kuanza kumuadhibu hadi
kupelekea mikono hiyo kufikia hatua ya kuoza kwasababu ya kukaa muda mrefu
ikiwa na majeraha kutokana na hilo mtoto huyo anaiomba serikali pamoja na watu
wenye moyo wa huruma waweze kumsaidia kwani hali yake siyo nzuri.
Mtoto huyo amesema baba
yake alifariki kwa kupigwa na wananchi kwa kusadikika kuwa ni mwizi lakini mama
yake yupo lakini amesha changanyikiwa kiakili kwahiyo muda wote amekuwa
akishinda katika vilabu vya pombe za kienyeji na amekuwa hana msaada wowote
kwake.
Kwa upande wake Kamanda
wa jeshi la jadi sungusungu katika mtaa wa Ibozya Magigo kata ya katoro ambapo mtoto huyo anaishi Bw.
Hamisi Twaha amesema kuwa watu wamrudie
mungu kwani kitendo hicho nicha kikatili na hakifai katika jamii kwani mtoto huyo inaweza kupelekea
kukatwa mikono yake yote miwili kutokana na mikono hiyo kuanza kuoza.
Kamanda huyo amesema
mtuhumiwa mpaka sasa ameshafikishwa katika kituo cha polisi katoro kwa uchunguzi zaidi.
Aidha mwenyekiti wa
mtaa huo wa Ibozyamagigo Bw. Mapambano Pasikali amelaani kutokea kwa kitendo
hicho na amewaomba watu wenye kuguswa na jambo hilo wajitokeza kumchangia mtoto
huyo kwani hali aliyo nayo ni mbaya sana
No comments:
Post a Comment