Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe akizungumza na
waandishi wa habari Mjini Dodoma (hawapo Pichani) kuhusu agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuachiwa huru kwa msanii wa Muziki wa kizazi
kipya Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego) Kulia ni Naibu Waziri wake Mhe.
Anastazia Wambura.
Akitoa kauli hiyo kwa
niaba ya Rais Magufuli, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Harrison George Mwakyembe amesema kuwa Msanii huyo ametumia haki yake ya
kikatiba ya kujieleza na ni Haki ya kila Mtanzania kujieleza kwa namna moja au
nyingine pasipo kuvunja katiba ya Nchi.
Waziri Mwakyembe
amesema Mwanamuziki huyo ni Mmoja kati ya wanamuzi wanaopendwa sana na Mhe Rais
kutokana na kazi zake za muziki zinazoelimisha na kueleza changamoto mbalimbali
zinakumba taifa letu.
“Mhe. Rais anaupenda wimbo
wa msanii huyu na ameshauri auboreshe zaidi asipunguze chochote ila aongezee tu
tabia nyingine ambazo hajazitaja katika wimbo wake” alisisitiza Dkt Mwakyembe.
Aidha Mhe. Waziri
ameeleza kuwa Mhe Rais ametoa ushauri kwa msanii huyo kuboreshe wimbo huo zaidi
kwani mengi aliyoyaongelea katika wimbo wake yanatokea katika jamii na kutolea
mfano kama akiboresha na kuelezea zaidi kuhusu wakwepa kodi,wauzaji,
wasambazaji na watumiaji madawa ya kulevya,na watanzania wasipoenda kufanya
kazi kwani makundi haya yote yapo katika jamii.
No comments:
Post a Comment