Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme akizungumza na wakazi wa
Kata ya Nala alipowatembelea na kusikiliza maoni na changamoto mbalimbali
zilizopo katika kuanza kutekelaza radi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa
Kimataifa Dodoma.
Diwani wa Kata ya Nala Mhe. Brayceon Leonard Eliah akiwasisitiza wakazi
wa Kata yake kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kutekeleza mradi huu wa
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa Dodoma
Bw.Salum Mkuya akitoa mrejesho wa
mambo yaliyofanywa na Kamati yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina
Mdeme(Hayupo Pichani) katika kuhakikisha Mradi huo
unafanikiwa.
Afisa Mipango Miji Manispaa ya Dodoma Bw. Clemence Msuva akieleza
taratibu za tathimini ya eneo lililopo katika Kata ya Nala utakapojengwa uwanja
wa Michezo wa Kimataifa zitavyofanyika ili kuwezesha mradi huo kuanza mapema.
Mmoja wa Mkazi wa kata ya Nala
Stanley Wilson akiuliza swali kwa Kamati Ndogo ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa kuhusu utekelzaji wa mradi huo na faida
watakazopata wakazi wa kata ya Nala na Dodoma kwa ujumla.
Mwanasheria kutoka
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy Kyando akiwahakikishia
wakazi wa Kata ya Nala kuwa Sheria na Taratibu zitafuatwa katika ulipaji wa
fidia kwao.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Nala wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
Mhe. Christina Mdeme(Hayupo Pichani) alipowatembelea na kusikiliza hoja
mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa
unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya
Dodoma Mhe. Christina Mdeme amewatahadharisha wakazi wa Kata ya Nala
watakaofanya aina yoyote ya udanganyifu katika ulipaji fidia kwao kwa ajili ya
mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa utaojengwa Mjini Dodoma.
Ameyasema hayo wakati
alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nala alipowatembelea na kusikiliza
hoja mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa
unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.
“Wewe kama unajijua
sio mkazi halali wa eneo unapopita mradi huu naomba ukafute jina lako ila
tukikubaini tutakuchukulia hatua kali za kisheria” alisisitiza Mhe. Christina.
Mhe. Christina Mdeme
ameongeza kuwa Serikali haipo tayari kupoteza hela kwa ajili ya kulipa watu
wasiostahili katika mradi huo na kwamba kila anayehusika kulipwa
fidia kihalali atalipwa.
Aidha Mhe. Christina
Mdeme amewahakikishia wakazi wa Kata ya Nala kuwa Serikali haitamdhulumu mtu
yoyote na atahakikisha kila anayepaswa kulipwa fidia analipwa fidia
anayostahili.
Pia amewatahadharisha
wakazi hao kutotumiwa na viongozi au vikundi vya watu kwa manufaa ya kujipatia
pesa zinazotokana na fidia za mradi huo kwa njia za udanganyifu.
Kwa upande wake
Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy
Kyando amewaomba wakazi wa Kata ya Nala kuwa watulivu na kwamba Sheria na
Taratibu za ulipaji fidia zitafuatwa kikamilifu katika zoezi hilo.
Akitoa maelezo ya kwa
niaba ya Kamati ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa
Kimatafa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw.Salum Mkuya amewahikikishia wakazi wa
Kata ya Nala ushirikiano kutoka kwa Kamati yake ili kufanikisha mradi huu wa
kimataifa.
Akizungumza
kabla ya kufunga mkutano huo Diwani wa Kata ya Nala Mhe. Brayceon Leonard Eliah
amewaomba wakazi wa Kata yake kutoa ushirikiano kwa maafisa wa Serikali
watakaokuwa wanatathimini maeneo yao kwa ajili ya ulipaji wa fidia.
No comments:
Post a Comment