Baadhi ya wananchi wakivuta kokolo wakipeleka eneo la kuchomea. |
Dhana haramu za uvuvi zikiwa zimekusanywa kwaajili ya kuchomwa kwenye mwalo wa dala dala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo. |
Meza kuu ikongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,wakisiliza kwa makini taarifa ambayo ilikuwa ikisomwa na afisa uvuvi. |
Afisa mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya
Mkoa wa Geita Shafii Ramadhan Kiteri,akitoa taarifa ya zoezi la oparesheni Tokomeza uvuvi haramu. |
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bi Janneth Mobe akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Nyasalala. |
Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,akizungumza na wananchi wa kijiji cha nyasalala juu ya wao kutoa ushirikiano kwa serikali katika kupambana na uvuvi haramu. |
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akizungumza. |
Zoezi la uchomaji wa dhana hizo za uvuvi likiendelea. |
Wito umetolewa kwa wananchi ambao wanafanya
shughuli za uvuvi Mkoani Geita,kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa
kuwafichua wale ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli ya uvuvi haramu katika
mialo iliyopo Mkoani Humo.
Rai hiyo
imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja
Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga wakati
wa zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi
kwenye Mwalo wa daladala uliopo
kijiji cha Nyasalala kata ya
Bukondo zilizokusanywa ndani ya miezi
miwili kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu.
Aidha mh Kyunga
amesema kuwa uhifadhi wa rasilimali zilizopo kwenye ziwa viktoria ni muhimu kwa
kila mwananchi kwani endapo uvuvi haramu
ukiachiwa madhara yake yanaweza kuwa ni makubwa kwa viumbe ambavyo vipo katika
ziwa.
“Ndugu
wananchi kwa kweli uhifadhi rasilimali zilizomo katika ziwa letu hili ni muhimu
,ni muhimu kwa sasa na vile vile kwa baadae isipokuwa mimi nisisitize sisi wote
hapa kwa ajili ya ustawi wetu na vizazi vijavyo tuone kwamba tuna wajibu wa kuhifadhi
mazingira na matumizi bora ya ziwa letu hili,tukilivuruga kama hawa wenzetu
wanavyolifuruga kwa kuendesha uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira hasara
ambayo wanatuachini ni kubwa sana hawa watu kwa lugha nyingine naweza kusema ni
wachawi”Alisema Kyunga
Hata hivyo
katibu wa BMU mwalo wa Daladala,Methusela
Samweli amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa changamoto kubwa ambayo wanapambana
nazo katika zoezi la kutokomeza uvuvi haramu ni
kukosekana kwa vitendea kazi ikiwemo kukosekana kwa Boti kutokuwepo kwa
ulinzi wa kutosha ambao utasaidia usalama wakati wa doria.
Karoli Makoba
na Baraka Mkwazu ni wananchi ambao wapo kwenye mwalo huo wameiomba serikali na
BMU kuweka uhusiano wa karibu kwa kushirikiano hili kutokomeza tatizo la uvuvi
haramu ambalo limeendelea kushamiri kwa kasi kubwa hususani kwenye mialo ya Izumacheli
na Mganza.
Kwa mujibu wa
maelezo ya afisa mfawidhi udhibiti ubora
wa samaki na usimamizi wa rasilima za
uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita Shafii
Ramadhan Kiteri,ameelezea kuwa Doria
ambayo imefanyika kwa miezi miwili
imefanikisha kukamata jumla ya samaki wachanga ambao
Kg 7,682,Mitumbwi 19,watuhumiwa 12,gari moja Hiace na Gari ya pili aina
ya Fuso Tandam,pikipiki 3,Nyavu za makila 1,261,Makokoro ya kuvutwa nchi kavu
23,Dududu 41na Timba 17.
Kiteri
ameongezea kuwa Katika doria hizo zote kiasi cha shilingi Milion,10,080,000
zimepatikana ambazo zimetokana na faini
mbali mbali ambazo walikuwa wakilipa watuhumiwa .
IMEANDALIWA
NA MADUKA ONLINE BLOG
No comments:
Post a Comment