Wananchi wa mtaa wa Nyantorontoro "A"Kata ya Nyankumbu wakikwa kwenye shughuli ya kujitolea ya utengenezaji wa Barabara. |
Shule ya Msingi ambayo wananchi wamejitolea kutengeneza Barabara ya kufika shuleni Hapo. |
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyantorontoro Gerevas Kayelelo kulia akifokeana na moja kati ya wananchi ambaye hakutaka eneo lake kuondolewa mihogo ambayo alikuwa amepanda. |
Elias Totoe mkazi wa nyantorotoro akizungumza namna ambavyo wameweza kufikia uwamuzi wa kutoa maeneo yao kwaajili ya maendeleo ya mitaa.
|
Lecta Maningu mkazi nyantorotoro akieleza juu ya tatizo la maji ambavyo limekuwa ni changamoto katika kata hiyo. |
Wananchi wakionesha vitendea kazi |
Gerevas Kayelelo m/kiti mtaa wa Nyantorotoro A,akifafanua juu ya uwamuzi wa wananchi kujitokeza kwenye shughuli ya utengenezaji wa barabara. |
Barabara ni moja Kati ya
huduma muhimu za kijamii zinazohitajika ili kurahisha na kuchochea
kasi ya maendeleo lakini maeneo yaliyo mengi hapa nchini yamekuwa
yakikabiliwa na changamoto ya miundombinu hiyo ambayo inarahisisha kasi ya
maaendeleo.
Kutokana na hali hiyo wananchi wa
mtaa wa nyantorotoro “A” kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita
wamejitokeza kutengeneza barabara ya kiwango cha molamu yenye
kilomita zipatazo mbili kuelekea kwenye taasisi ya shule mpya ya mtaa huo.
Baadhi ya wananchi
wamezungumza na mtandao wa Maduka Online na kwamba wamejitolea kutengeneza
Barabara kwa ushirikiano ni kutokana na muda mrefu kutokuwepo kwa
barabara na shule kwenye mtaa huo.
“Kiukweli watoto wetu wamepata
shida kwa muda mrefu na kusoma umbali wa kilomita nyingi kutokana na shule
kukamilika tumeonelea basi sisi pamoja na mwenyekiti wetu wa mtaa kuweka
jitihada za kutengeneza barabara ambayo itaelekea shuleni na itawasaidia watoto
wetu kutembea kwa ukaribu kufuata elimu”alisema Lecta Maningu.
“Pamoja na kwamba sisi kama
wananchi tumejitolea kujenga barabara ambayo inaelekea shuleni lakini tunaiomba
serikali yetu kupitia kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji kuona umuhimu wa
kuweka maji shuleni hapo ili kupunguza adha kwa wanafunzi shuleni hapo kwani
hakuna maji”aliomba Bi, Cesilia Clement
Lakini pamoja na baadhi ya
wananchi kutoa maeneo yao kwa hiyari ili kupitisha barabara, wapo wengine
wanakwamisha juhudi za wengi kufikia malengo hayo, kama mzee aliyetambulika kwa
jina la Mayenga ambaye ameonekana mgumu wa kutoa eneo lake lililolimwa
mihogo jambo ambalo limesababisha malumbano makali baina yake na wananchi.
Mwenyekiti wa Mtaa huo Gerevas
Kayelelo, alisema kuwa wananchi wake wametoa ardhi yao kwa ajili ya barabara
bila kuomba hata fidia ya aina yoyote.
Mpaka storm inaondoka katika mtaa
huo imeacha wananchi wakiendele na ujenzi wa barabara kwenye Shamba la
Mzee Mayenga lenye ukubwa wa mita 150.
No comments:
Post a Comment