Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl. Herman Kapufi.
Serikali wilayani na mkoani
geita imesema haita walipa fidia wananchi watakao bomolewa nyumba zao au
kukatiwa miti pindi zoezi la usambazaji wa nguzo za umeme
vijijini litakapo kuwa limeanza kutekelezwa.
Hatua hiyo imekuja
baada ya kuwepo kwa maeneo mengi wilayani geita ambayo hayajapatiwa
umeme kutokana na miundo mbinu kuwa duni ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za
makazi kiholela jambo ambalo limesababisha shirika la umeme tanzania (TANESCO)kushindwa kupitisha nguzo
kwasababu hiyo.
Akizungumza na
wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro mkuu wa wilaya ya Geita Hermani Kapufi amesema kuwa
serikali itapeleka nguzo maeneo ambayo hayajapatiwa umeme kutokana na hilo
hakuna mwananchi atakae lipwa fidia kama nyumba au miti yake itakuwa kandokando
ya ramani ambapo nguzo za umeme zinatarajia kupita katika maeneo hayo.
Aidha kapufi amewataka
wananchi walio tandaza nyaya katika nyumba zao wategemee kufungiwa umeme mwezi
wa tatu na wanne na kwa wale ambao hawaja tandaza nyaya katika nyumba zao
waweke ili zoezi hilo lifanyike kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment