Sunday 5 March 2017

WASANII WA FILAMU WAMETAKIWA KUUNGANA NA KUWA KITU KIMOJA MKOANI GEITA

Meneja wa NSSF Mkoani Geita  Shabaan Mpendu akizindua na kuonesha Filamu ya Walimwengu iliyochezewa Mkoani Geita ambayo imezinduliwa jana kwenye ukumbi wa hotel ya Lenny.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifatilia matukio kwa umakini zaidi.

Moja kati ya wasanii wa nyimbo za RNB Mkoani Geita akitoa burudani wakati wa uzinduzi.

MC wa shughuli mwanadada Rose Mweko akiwaita wasanii wa Maigizo kwaajili ya burudani.

Moja kati ya kikundi cha sanaa ya maigizo Mkoani Geita kikitoa burudani ya uchekeshaji .

Mgeni Rasmi ambaye ni Meneja wa Nssf Mkoani Geita akizindua DVD ya Walimwengu.

Afisa Mazingira Halmashauri ya Mji wa Geita Pancras Shwekerera akiwasisitiza wasanii wa Maigizo kuwa na moyo wa kujituma bila ya kurudishwa nyuma na maneno ya watu. wakati wa uzinduzi wa  DVD ya Filamu ya Walimwengu.

Meneja wa NSSF Mkoani Geita  Shabaan Mpendu ,akiwasisitiza wasanii kujiunga na umoja wa wasanii ili waweze kutambulika na serikali kwani utawasaidia kupata misaada zaidi.

Wageni baadhi wakifatilia kwa umakini zaidi.

Baadhi ya wasanii wakiwa kwenye meza ya pamoja wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasimi.

Waandishi wa habari wakifatilia matukio yaliyokuwa yanajiri.

Wasanii wakifurahia na kucheza kwa pamojaa.

Mwenyekiti wa chama cha waigizaji Mkoani Geita,Rose Michael(Rose Bonanza )amewahasa wasanii kuachana na maneno yasiyokuwa na manufaa kwao na kufanya kazi ya sanaa kwa malengo ya ajira sio sehemu ya kupotezea muda na majaribio ya maisha .

Moja kati ya wasanii wa Maigizo Mkoani Geita,Sagari Mganga akicheza igizo ambalo lilikuwa linapiga vita dhadi ya mfumo dume katika familia.

Akisoma risala mbele ya Mgeni Bw,Ahamed Seif  amesema  Pamoja na wasanii kuwa na jitihada ya kuingia katika fursa ya ajira kwa njia ya kuigiza bado wanakumbana na changamoto zinazowakatisha tamaa ambapo msoma risala Ahmed Seifu anasema wanakumbana na changamoto ya ufinyu wa bajeti,kukosa sapoti kwa wadau mbalimbali pamoja na masharti magumu kwao wanayopewa na wanunuzi wa filamu.

Baadhi ya Wasanii walioshiriki katika filamu ya Walimwengu.


Meneja wa NSSF Mkoani Geita  Shabaan Mpendu,akisoma maelezo yaliyokuwepo kwenye check ambapo kwa kudhamini na kutambua mchango wa wasanii alitoa kiasi cha sh,milion 3.

Meneja wa Leny Hotel akitoa neno kwenye uzinduzi huo.

Katibu wa chama cha waigizaji jijini Mwanza Edwin Kimbulu akitoa mchango wao kwa niaba ya wasanii wa jiji la Mwanza.

Afisa Mazingira Halmashauri ya Mji wa Geita Pancras Shwekerera akinunua DVD ya Filamu ya Walimwengu.

Michael Kapaya Msanii aliyecheza Filamu ya Walimwengu akishukuru kwa Wageni waliohudhuria huku bado akiiomba Serikali kuharakisha kukamilisha sera ya maendeleo ya filamu ambayo inategemewa kuwa mwarobaini wa changamoto zinazoikabili sekta hiyo yenye kutoa ajira kwa vijana wengi nchini.



No comments:

Post a Comment