Shirika
lisilo la kiserikali la Plan International Mkoani Geita limekabidhi kituo cha
malezi na makuzi ya awali kwa watoto wadogo chenye thamani ya sh,milioni
thelathini na nne laki nne na elfu tatu
mia nne na tisini katika kata na kijiji cha Magenge wilayani hapa.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo na serikali ya kijiji,yaliyofanyika leo meneja wa Plan
Mkoani humo Gratian Mushema Kweyamba,alisema kuwa lengo la ujenzi wa kituo
hicho ni kumsaidia mtoto ambaye yupo chini ya umri wa miaka sifuri hadi miaka mitano (5) ambapo anaweza kujifunza mambo mbali mbali
ya msingi.
“Tunaamini
kuwa kituo hiki kitawasaidia watoto kupata elimu ya kujitambua wakiwa bado
wadogo na ndio maana kauli mbiu yetu tunasema plan watoto kwanza, tunaamini kuwa mtoto akijengewa misingi mizuri
pamoja na malenzi yaliyomema anaweza
kuwa msaada kwa serikali na jamii inayomzunguka”Alisema Kweyamba.
Akielezea
mafanikio ya ujenzi wa mradi huo,msimamizi wa kituo Bi,Lydia Wanjala,amefafanua
kuwa tangua waanze ujenzi wamefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutokana na jamii ambayo ipo eneo husika kutoa ushirikiano kwa kiasi kikubwa .
Akimwakilisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ,Afisa ustawi wa jamii ambaye ndiye alikuwa
mgeni rasmi kwenye makabidhiano hayo Anderson Shimbi
aliwashauri wanakijiji kuwa waangalizi wa mradi huo na kuutunza kwa
uangalizi mkubwa zaidi.
“Ndugu zangu
wanakijiji gharama iliyotolewa hapa ni kubwa sana hivyo tunatakiwa sisi wenyewe
tuwe watu wa kwanza katika utunzaji wa
mali hizi zilizopo kwenye kituo hiki”alisema Shimbi.
Diwani wa
kata ya Magenge,Edward Misungwi,ametoa ahadi ya kuhakikisha wanakuwa walinzi
wakubwa wa mradi huo na kwamba kwa mwananchi ambaye ataonekana kukiuka masharti yaliyowekwa hatua
kali zitachukuliwa dhidi yake.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
No comments:
Post a Comment