Wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro
wilayani na mkoani Geita wameiomba Serikali
kupiga marufuku uuzaji wa silaha za jadi kiholela ili kuepuka madhara yanayo
weza kujitokeza katika jamii kutokana na silaha hizo kuuzwa pasipo kufuata
utaratibu.
Wakizungumza baadhi
ya wananchi hao wamesema kuwa kumekuwepo na idadi kubwa ya watu katika eneo
hilo ambao wanajishughulisha na biashara
hiyo ya uzaji wa silaha za jadi kiholela jambo ambalo linahatarisha usalama wa
watu kutokana na silaha hizo kufikia
hatua ya kupangwa kandokando ya barabara
na kwenye mirundikano mikubwa ya watu
ikiwa ni pamoja na kwenye viwanja vya michezo.
Aidha wamezitaja silaha zinazo uzwa katika maeneo hayo ni pamoja na
mikuki , mishale, visu,shoka, sime pamoja na mapanga.
Kwa upande wao wafanya biashara wa silaha hizo Bw.
Masalu Rukasi na Gervas Manyilizu wameeleza kuwa kabla ya kuingiza sokoni zana
hizo kwa ajiri ya biashara wanakuwa na
kibali kutoka kwa kiongozi wa eneo husika kwa sababu ya usalama zaidi.
Wafanyabiashara hao wamesema kumekuwepo na baadhi ya watu wanao kiuka
taratibu hizo ambazo wanatakiwa kufuata
na badala yake huuza zana hizo kihole
kitendo ambacho kinahatarisha usalama wa raia katika jamii.
aidha mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa katoro Japheti Madoshi amewataka wanao jishughulisha
na biashara hiyo kandokando ya barabara na kwenye mirundikano mikubwa ya watu
waache mara moja na badala yake watafute
sehemu iliyo salama kwa ajiri ya biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kujenga
vibanda vya kuhifadhia zana hizo.
No comments:
Post a Comment