Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi ameteketeza na kuvuruga shamba la Bangi ambalo linasadikika kuwa na ukubwa wa hekari mbili na nusu la Bangi huku akisisitiza kuwa hakuna mtu yoyote atakeyepona ndani ya Wilaya yake iwapo atabainika anajihusisha na madawa ya kulevya ambayo yamekuwa ni hatari kwa vijana wengi.
Mkuu huyo wa Wilaya alitoa kauli hiyo jana wakati wa zoezi la kuteketeza kwa moto mimea ya bangi kwenye shamba ambalo lipo Mtaa wa Samina B kata ya Mtakuja iliyopo halmashauri ya Mji wa Geita.
Kapufi alisema vijana wengi wanaokaa kwenye vijiwe wanaangamia kwa uvutaji wa bangi na kwamba watu wanaojishughulisha na ulimaji pamoja na usambazaji hatasita kuwachulia hatua kali za kisheria, huku akitoa rai kwa wananchi kuwafichua wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.
‘’Ndani ya Wilaya yangu sitasita kuwachulia hatua watu wote wanaojihusisha na ulimaji ikiwemo usambazaji wa madawa ya kulevya hatuwezi kuona vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa wakiteketea kwa madawa hatutakubali…lakini niwashukuru wananchi waliotupatia taarifa kuwepo kwa shamba hili ambalo leo [jana] tunachoma motomimea ya bangi’’alisema Kapufi.
kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa samina B. John Balenge alisema kuwa walipata taarifa za shamba hilo la bangi kutoka kwa wananchi waliokuwa wakienda porini kufanya shughuli za kutafuta kuni na mkaa na kwamba waliweka mtego wa kumnasa mwenye shamba bila mafanikio.
‘’Ndugu waandishi kama mnavyoona shamba hili linaonesha mwenye nalo alikuwa akilitunza limesafishwa vizuri niseme tu sisi tulipata taarifa kwa wananchi tukawa tunaweka ulinzi wa kumkamata mmiliki ni mwezi sasa bila mafanikio,’’alisema mwenyekiti huyo.
Naye diwani wa kata ya Mtakuja ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa geita Constatine Morand alisema hayuko tayari kumuona mtu akifanya biashara ya madawa ya kulevya katika kata yake na kwamba wanamuunga mkono rais katika vita hiyo.
‘’Nitowe wito kwa wananchi wote wa kata ya Mtakuja siko tayari kuona biashara hii ikiendelea kwenye kata yanngu na kuangamiza watanzania wengi…na sisi huku chini tunamuunga mkono rais wetu Dk. John Magufuli katika vita hii waliyoianzisha,’’alisema morandi.
Akizungumza na MADUKA ONLINE mmoja katti ya vijana ambao walikuwa wakitumia Bangi hapo zamani na kuamua kuachana nazo ,Juma Suleiman alisema madawa hayo ya kulevya hayana faida yoyote na badala yake yanatia hasara kwa vijana na kurudisha maendeleo nyuma.
Kutokana na biashara hii ya bangi kushamiri katika visiwa vilivyoko mwambao wa ziwa victoria, Mkuu wa Wilaya alisema wakimaliza oparesheni maeneo ya nchi kavu watahamishia nguvu majini kwenda kupambana na wafanyabiashara wa zaohilo haramu.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
No comments:
Post a Comment