Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuzuia timu za
Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu
uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye
akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na
Serikali kufikia uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa
kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika
Oktoba Mosi 2016.
Timu za soka za Simba
na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda
usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa miumbombimu ya
Uwanja wa Taifa yakiwemo mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa
viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.
Uamuzi huo umetolewa
leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akikagua na kutembelea maeneo
yalioathirika na uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba na Yanga katika mechi
iliyochezwa Octoba Mosi 2016 katika Uwanja wa Taifa.
“Hii si mara ya kwanza
kwa mashabiki kuvunja mageti na kung’oa viti na sisi kama Serikali tumeamua
kuzuia vilabu hivi vya Simba na Yanga kutotumia Uwanja wa Taifa mpaka
tuitavyoamua vinginevyo hapo baadae” Alisistiza Mhe. Nnauye.
Mhe. Nape Nnauye
ameongeza kuwa wameendaa mfumo wa kutumia kamera Uwanjani ili kubaini makosa
yatakayokuwa yanafanyika ili kuzuia vitendo vya kihualifu na uharibifu katika
Viwanja vya michezo.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa
wamesikitishwa sana na uharibifu ulitokea katika mechi ya Simba na Yanga na
kusababisha uharibifu wa viti na mageti ya kuingilia Uwanjani.
Ameongeza kuwa kwa
tathimini iliyofanyika mageti manne yameng’olewa na mashabiki kwa upande wa
Simba na Yanga na pia kwa upande wa ndani jumla ya viti 1781 vimeng’olewa
katika upande wa mashabiki wa Simba.
“Mara nyingi
tumekubaliana kutunza Uwanja huu kwa ajili ya matumizi ya watanzania wote na
kama wasimamizi tunasikitika kwa kitendo hiki kilichotokea na tujue kuwa ni
kodi za wananchi ndio zilitumika kujenga Uwanja huu na pia ndizo zitazotumika
kukarabati Uwanja tuwe na tabia ya kupenda na kutunza vya kwetu.
Klabu za Simba na
Yanga zimekuwa na ushindani mkubwa katika soka la Tanzania na kumekuwa
kukitokea mambo mbalimbali pale timu hizo zinapokutana ikiwemo uharibifu wa
miundombinu katika Viwanja na vurugu kwa mashabiki pale mmoja wao anapofungwa.
No comments:
Post a Comment