Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo ya ujenzi wa
kivuko kipya cha Mv Kazi kutoka kwa Mkandarasi wa Kivuko hicho Mhandisi Major
Songoro wa Kampuni ya Songoro Marine Boat Yard.
Kivuko Kipya kwa ajili ya
Magogoni/Kigamboni kitakachoitwa MV. Kazi kikiwa katika hatua za awali za
Ujenzi wake. Kivuko hiki kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 170 sawa na abiria
800 pamoja na magari 22 kwa wakati mmoja.
Sehemu ya juu (deck) ya
kivuko kipya cha Mv Kazi ikiendelea kujengwa. Kivuko hiki kitakuwa na uwezo wa
kubeba tani 170 sawa na abiria 800 pamoja na magari 22 kwa wakati mmoja.
Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Kulia) akitoa Maelekezo kwa
kuhusu upatikanaji kwa haraka kwa Kivuko cha Mv Kazi ili kurahisiha
huduma ya vivuko kwa JJijji la Dar es Salaam na vitongoji vyake wakati
alipotembelea kujjionea ujenzi wa kivuko hicho. Wa pili kutoka kushoto ni
Mhandisi Jamal Waziri na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dr. Musa Mgwatu.
Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akifafanua Jambo kwa Abiria
wanaotumia vivuko vinavyotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni alipotembelea
Kivukoni hapo. Wa nne kulia waliosimama ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dr. Musa
Mgwatu.
Abiria wakishuka katika
Kivuko cha MV. Magogoni upande wa Kigamboni, Kivuko cha Magogoni kilifanyiwa
ukarabati mkubwa mwezi Mei 2016 na sasa kinaendelea kutoa huduma kwa wananchi
wanaotumia kivuko hicho.
No comments:
Post a Comment