Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini
Prof.Justin Ntalikwa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi
kiuchumi Bi.Beng’i Issa wakipata maelezo toka kwa Bi Shamsa Diwani wa
kikundi cha MIVA kinachojiusisha na uchimbaji mdogo wa madini na usio rasmi leo
jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano
kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini.
Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa
uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i
Issa wakipata maelezo toka kwa Bi Susan Fred wa TAMICUSO ambao wanajiusisha na
uchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini
Prof.Justin Ntalikwa akiuliza swali kwa Bi Martha Kayaga wa kikundi cha
WAWACHISI tokea singida jinsi wanavyochimba madini ya gypsum na kuyahifadhi
katika mkutano wa wadau wanawake katika sekta ya madini.Kulia ni Katibu
Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi
kiuchumi Bi.Beng’i Issa akizungumza na
wanawake wachimbaji madini wadogo wadogo(hawapo pichani) leo katika ukumbi wa
Mwalimu Nyerere walipokutana katika mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta
ya madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini
Prof.Justin Ntalikwa akizungumza jambo na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa
uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i
Issa,Bi Tertula Swai wa UN women na Kessy Edward wa Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi
kiuchumi.
Profesa Ntalikwa ameyasema hayo wakati akifungua
mkutano kazi wa wadau wanawake katika
sekta ya madini wanaojihusisha na uchimbaji ambao sio rasmi na mdogo uliofanyika
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Mimi wito wangu kwa wachimbaji hawa ni kwamba
nawaomba wajipatie elimu na teknolojia sahihi ili waweze kujiongezea kipato
katika uchimbaji huu”,Alisema Prof Ntalikwa.
Aidha Katibu Mkuu uyo aliwataka wachimbaji wadogo
wadogo hao kuwasiliana na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC)
kwa ajili ya kuwasaidia sehemu ambazo ambazo wanaweza kupata mitaji maana suala
la mtaji ni muhimu sana ili waweze kuboresha shughuli za uchimbaji.
Pia amesema kuwa serikali imeanza kutoa ruzuku kwa awamu kwa
wachimbaji hawa wadogo wa madini na hivi sasa wanajipanga kutoa awamu ya tatu
ya ruzuku ikiwa na lengo ya kuwasaidia
kununua vifaa vya uchimbaji na teknolojia sahihi itakayorahisisha uchimbaji wa
madini na kuongeza kuwa kwa sasa wameshapokea maombi kutoka kwa wachimbaji
mbalimbali na wanayafanyia kazi ili wapate washindi watakaojipatia ruzuku.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa
uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i
Issa amesema kuwa wao kama baraza watatengeneza programu ya jinsi ya kupata
uongozi kwa wachimbaji hao ambao utasaidia kuwakilisha mawazo yao serikali na
pia program ya kuwajengea uwezo pale ambapo wachimbaji hawa wana mapungufu na
pia kuwaunganisha na masoko kama vile viwanda vya ndani ili visinunue malighafi
kutoka nje na badala yake wanunue hapa nchini malighafi yanatotokana na
uchimbaji wa madini.
No comments:
Post a Comment