Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu
Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya
Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na
kilelele chake kukoma Oktoba 6, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali ndani nje ya nchi
wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama
Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele
chake kukoma Oktoba 6, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu,
Dkt Mwele Malecela akizungumza mapema leo, alipokuwa akimkaribisha Makamu wa
Rais Mama Samia Suluhu Hassan,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 lililoanza
leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Katika kongamano hilo
kauli mbiu yake ni “Uwekezaji katika tafiti zenye ubunifu ili kufikia malengo
endelevu ya dunia.”.
Dkt Mwele alieleza pia
Mada zitakazojadiliwa ndani ya kongamano hilo kuwa zitajikita zaid kwenye
maeneo kama vile 1. Mkakati wa kuboresha afya ya uzazi, ya mama, watoto
wachanga na vijana. 2. Magonjwa sugu yasiyoambukiza na changamoto zake,3.
Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua
kikuu na malaria,4. Usalama wa Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi,5.
Mkakati wa afya moja katika kudhibiti magonjwa ya milipuko,pamoja na 6.
Magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na
nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya
200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala,alipokuwa akiwasili
katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
leo, kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu(NIMR), pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa
ya Binadamu Dkt Mwele Malecela,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo kufungua Kongamano la 30
la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kati ni
Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Hamis Kigwangala.
No comments:
Post a Comment