Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoa wa Shinyanga inazidai Halamashauri, Mashirika na Taasisi za Serikali mkoani humo jumla ya shillingi 163,269,269.82 kutokana na kupata huduma ya matengenezo ya magari.
Katika taarifa yake
kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali
amesema madeni hayo ni ya mwaka wa fedha 2016/2017 na wamesha wasilisha madai
yao kwa wahusika na wanasubiri kulipwa.
Mhandisi Riziki Lukali
aliwataja wadaiwa hao kuwa ni TANROADS Shinyanga Sh 24,193,733.21,
TANESCO Shinyanga Sh Milioni 96,267,987.63, DED Kishapu Sh
6,753,735.03, RAS Shinyanga Sh 2,742,097.36, KUWASA Kahama Sh 9,855,714,
KASHUWASA Shinyanga Sh 1,992,430, TBA Shinyanga Sh 5,103,062.56, Mahakama Kuu
Shinyanga Sh 5,470,628.91, Uhamiaji Shinyanga Sh 896,333.63, DAS Kishapu Sh
1,071,573.57, NSSF Shinyanga Sh3,798,184 pamoja na RMO Shinyanga shilingi
5,123, 789.92 milioni na jumla ya madeni hayo yote ni Sh 163,269,269.82.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu
amefurahishwa na utaratibu wa TEMESA Shinyanga wa kuzuia magari ya
taasisi, halmashauri na mashirika yanayodaiwa na kituo hadi hapo yatakapolipiwa
gharama za matengenezo.
Na pia amemuagiza Meneja
wa TEMESA Shinyanga kutoa taarifa kwake kama kuna Taasisi za Serikali ambazo
hukiuka Sheria kwa kutopeleka magari yake kwenye karakana za TEMESA na kupeleka
magari hayo kwenye karakana binafsi zilizomo mkoani humo ili hatua stahiki
ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Dkt Mgwatu amesisitiza
watumishi kuendelea kujituma kufanya kazi kwa weledi na kwa ubora zaidi ili
karakana iweze kuvuta wateja wengi na kuongeza pato la kituo.
Aidha TEMESA Shinyanga
kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 kituo kimepanga kukusanya jumla ya Sh
458,160,000 kutokana na madeni na huduma zinazoendelea kutolewa kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya
kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo Kanda ya Ziwa ili kubaini changamoto mbali
mbali zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment