Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelaani kitendo cha wanakijiji
kuwaua watumishi wa Serikali waliokuwa wakifanya utafiti wilayani Chamwino
mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Oktoba 3,
2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni
sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na makundi mbalimbali.
Mauaji ya watafiti hao, Teddy
Nguma, Jafari Mafuru na dereva wao Bw. Nicas Magazine yalitokea Oktoba Mosi,
2016 baada ya kushambuliwa na wakazi wa kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino
mkoani Dodoma.
Amesema Serikali imesikitishwa na
mauaji ya watu watatu wakiwemo watafiti wawili kutoka Kituo cha Utafiti wa
Kilimo cha Seliani (SARI) kilichopo mkoani Arusha ambao walikuwa kazini
kuchunguza sampuli za udongo ili kubaini kama matetemeko yataendelea kutokea.
“Kutokana na tetemeko lilitokea
mkoani Kagera, Serikali iliamua kushirikisha watalaamu mbalimbali kufanya
uchunguzi kuona kama tetemeko hilo ni endelevu au la katika maeneo mengine.
Kitendo cha watu kujichukulia hatua mkononi na kukatisha uhai wa watumishi
ambao walikuwa kazini hakikubaliki,” Alisema
Amesema watalaamu hao walifika
katika Wilaya ya Chamwino na kufanya kazi kwa siku tano na siku ya sita ndipo
walipoenda eneo la kijiji cha Iringa Mvumi kuendelea na kazi ambapo waliuawa
wakiwa kazini.
“Serikali kupitia kamati ya ulinzi
na usalama ya mkoa inaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watu waliofanya kitendo
hicho’’ Alisema
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewatoa
wasiwasi watumishi wanaohamia Dodoma kuwa Dodoma ni salama na kila anayekuja
yupo salama. “Dodoma ipo salama na tunatarajia kila anayehamia hapa atakuwa
salama na hata wakazi wa hapa wataendelea kuwa salama,’’
No comments:
Post a Comment