Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefanya mabadiliko makubwa kwenye Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, akiwabadilisha wabunge ishirini na wanne waliokuwa wanaunda kamati hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, Ndugai ameteua wajumbe wapya kumi na sita wa kamati hiyo ambao pia watakuwa wajumbe wa kamati nyingine.
Taarifa hiyo imeeleza
kuwa Spika ametumia Mamlaka aliyonayo kikatiba kuunda Kamati za Bunge kadri
anavyoona inafaa, na kwamba mabadiliko haya yamelenga katika kuboresha
utekelezaji wa majukumu ya kibunge.
“Kanuni ya 116 (3) –(5) ya Kanuni za Kudumu za
Bunge, Toleo la Januari 2016 inampa Spika mamlaka ya kuteua wajumbe ili wawe
wajumbe katika kamati mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na mamlaka ya
kuongeza, kubadilisha au hata kupunguza idadi ya wabunge katika kamati za
kudumu za Bunge,” imeeleza taarifa hiyo.
Mabadiliko hayo
yameanza mara moja kuanzia mwezi huu wa Oktoba na kwamba wajumbe wote
wameshatumiwa barua tayari kwa maandalizi ya kukutana na kuwachagua viongozi wa
kamati hiyo.
Hii ni orodha ya
waliokuwa wajumbe wa kamati hiyo na kamati walizohamishiwa kufuatia mabadiliko
hayo:
No comments:
Post a Comment