Wanawake wanne na
wanaume tisa wamefikishwa mahakamani mjiniDodoma na kusomewa mashtaka ya
mauaji ya watafiti wa Chuo cha Utafiti wa Udongo na Maendeleo ya Ardhi
kilichopo Selian mkoani Arusha.
Mbele ya Hakimu Mkazi,
Joseph Fovo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Dodoma haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama
Kuu.
Wanadaiwa kuwaua Nicas
Mag- azine, Theresia Nguma na Faraji Mafuru, Oktoba Mosi kwenye Kijiji cha
Iringa Mvumi wilayani Chamwino.
Wakili wa Serikali,
Beatrice Nsana aliwasomea mashtaka hayo jana akidai walitenda kosa hilo la
jinai kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na
marekebisho yake ya mwaka 2002.
Washtakiwa hao ni
Cecilia Mwalu, Dorca Mbehu, Edna Nuno, Grace Masaulwa, Juma Madeha, Albert
Chimanga, Sosteness Mseche, Julius Chimanga, David Chimanga, Lazaro Kwanga,
Yoramu Samamba, Edward Lungwa na Simon Samamba, wote wakazi wa Kijiji cha
Iringa Mvumi.
Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika.
No comments:
Post a Comment