Mtendaji Mkuu TEMESA
Mhandisi Mussa Mgwatu (kushoto) akisikiliza taarifa ya kituo cha TEMESA Mkoa wa
Mwanza kutoka kwa Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
Abiria wakiteremka katika Kivuko cha Mv Kome II kinachotoa huduma kati
ya Nyakarilo na Kome wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Mtendaji Mkuu TEMESA
Dkt. Mussa Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo
kuwafuta kazi mara moja watumishi sita wa kivuko cha Mv Kome kuanzia 11/10/2016
pamoja na kuwapa onyo kali watumishi wengine wawili wa kivuko hicho kwa
kuondoka katika eneo la kazi bila ruhusa ya mkuu wao wa kazi.
Ametoa agizo hilo
wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha TEMESA mkoani Mwanza na
kutembelea kivuko cha Mv Kome kinachotoa huduma ya usafiri kati ya Kome na
Nyakarilo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Dkt Mussa Mgwatu pia
amemwagiza Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo kuhakikisha
wafanyakazi wa karakana na kivuko wanawajibika ipasavyo ili kuondoka na uzembe
kama uliojitokeza.
“Hatuwezi kuvumilia
uzembe namna hii watumishi wanaamua tu kuondoka eneo la kazi bila kupata ruhusa
kutoka kwa wakuu wao hii sio sawa kabisa na nakuagiza Meneja hawa watumishi
waache kazi mara moja” alisisitiza Dkt Mgwatu.
Aidha Dkt Mussa Mgwatu
amemwagiza Meneja wa TEMESA Mwanza kuajiri watumishi wengine ili kujaza nafasi
zilizoachwa wazi kwa kuzingatia weledi na uwajibikaji wawatumishi watakao waajiri.
Kwa upande Meneja wa
TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo alikiri kuwa hakukuwa na ruhusa yoyote
ya maandishi iliyotolewa kwa watumishi kutokuwepo kazini siku hiyo.
“Mtendaji sina barua
yoyote kutoka kwa watumishi hawa iliyofika kwangu kuomba ruhusa ya kutokuwepo
katika kituo cha kazi.” alisisitiza Mhandisi Mishamo.
Mhandisi Ferdinand
Mishamo amewaja watumishi waliachishwa kazi kuwa ni walinzi
wanne Bw. Apolinary Kapulula, Bw. Marwa Nchagwa , Bw. Msomi Stanley na Joseph
Mtokambali, wengine ni Bw. Baharia Geofrey Biseko na Mkusanya Mapato wa kivuko
hicho Bw. Elisha Mbondo.
Amewataja Watumishi
wanaopewa onyo kali ni Mkuu wa Kivuko cha Mv Kome Bw.Elias Mabushi na dereva wa
kivuko hicho Bw.Juma Bugingo.
Dr.
Musa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo Kanda ya
Ziwa ili kubaini changamoto zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment