Mkuu wa Wilaya mhe.Josephat Maganga
ameelekeza wakuu wa shule kushirikiana na bodi ya shule kuandika taarifa ya
matukio ya ujauzito yanayotokea katika shule zao na kuhakikisha zinafika ofisi
ya afisa elimu wilaya ambapo ataipeleka ofisi ya Mkuu wa wilaya, pia walimu
wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ya Ualimu,
“bahati nzuri nilishawahi kuwa mwalimu
katika chuo cha Ualimu, nikapanda ngazi na kuwa afisa elimu Wilaya
Serengeti,Biharamulo na Chato, kutokana na kufanya kazi kwa kusimamia kanuni na
sheria nikapanda na kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Butiama, na sasa ni Mkuu wa Wilaya hakika nitaendelea kusimamia na kutekeleza
kanuni na sheria “alisema Maganga.
Alisisitiza kila mwalimu anawajibu wa
kuhakikisha mwanafunzi anayeanza shule anasimamiwa vizuri mpaka anamaliza shule
na walimu kuacha kukaa kimya wanapopata matatizo.
Baada ya semina elekezi Mkuu wa
Wilaya ya Bukombe mhe. Josephat Maganga ameagiza wakuu wa shule, waratibu elimu
kata kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi, pili walimu kuhakikisha
wana kanuni na sheria, tatu daftari la adhabu shuleni, mwisho wanafunzi wa kike
kuchunguzwa ujauzito kila baada ya miezi mitatu (3) na Maafisa elimu wilaya
kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia utekelezaji wa maagizo hayo.
No comments:
Post a Comment