Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Imeelezwa kuwa asilimia
30 ya vifo vyote nchini vinavyotokea kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 15 na
kuendelea, vinatokana na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza kama vile kisukari,
saratani, msukumo wa damu na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam
leo Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Magonjwa yasiyo ambukiza Tanzania,
Dkt. Andrew Swai amesema, ili kuepukana na magonjwa ya aina hiyo Serikali
kupitia wataalam mbalimbali wa afya wanawajibu wa kuhakikisha wanatoa elimu ya
kutosha kwa umma juu ya athari na namna ya kukabiliana na magonjwa hayo
Amesema magonjwa hayo
yanasababishwa na mtindo wa maisha hasa kutokufanya mazoezi ya mwili pamoja na
kutumia vitu vyenye sukari na chumvi nyingi.
Dkt. Swai amesema kati ya
magonjwa hayo, ugonjwa wa 'presha' unaonekana kuongoza kwa vifo kwani ugonjwa
huo husababisha vifo kwa asilimia 27 kutokana na kutokuwa na dalili na mara
nyingine watu kuhisi kuwa wamerogwa.
Chama cha Madaktari wa Magonjwa
yasiyo ambukiza Tanzania kimetoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuwa mstari
wa mbele katika kuhakikisha wanaripoti na kuandika taarifa za magojnwa hayo
kwani ndio yanaogoza kwa kusababisha vifo.
No comments:
Post a Comment