Mkuu wa Wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizindua maktaba ya
kisasa iliyopo shule ya wasichana ya nyakumbu iliyopo kata ya Nyakumbu.
Msemaji wa shirika lisilo la Kiserikali la Read International
Stella Mtega,akishukuru kwa GGM kwa kufanikisha kutoa fedha ambazo zimesaidia
kununua vitabu kwaajili ya maktaba.
Afisa mahusiano wa GGM Manase Ndoloma akiwaeleza wanafunzi
wa shule ya sekondari ya wasichana nyakumbu umuhimu wa
kupenda kusoma vitabu ni kwenye uzinduzi wa maktaba katika shule hiyo ulio
fanyika leo tarehe 17 Oktoba.
Jumla ya kiasi cha sh milioni ishirini (20) kimetolewa na mgodi wa
dhahabu wa Geita (GGM) kwenye shule ya Sekondari ya wasichana ya Nyankumbu
iliyopo wilayani na mkoani Geita lengo ikiwa ni kuweka vitabu vya kutosha
katika maktaba ya shule hiyo.
Akizungumzia changamoto ambazo walikuwa wakikutana nazo wanafunzi wa
shule hiyo,Hajira Salum na Verediana Traphone wamesema kuwa changamoto ya uhaba
wa vitabu shuleni hapo ilikuwa ni moja wapo ya kikwazo kilichokuwa
kikisababisha wanafunzi kutokufanya vizuri shuleni hapo .
Aidha kwa upande wake Afisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa GGM
Manase Ndoroma,amewasisitiza wanafunzi hao kujenga desturi ya kusoma kwa bidii
vitabu ili kuendana na Dunia ya sayansi na teknolojia.
“Tunatambua kuna faida nyingi sana katika kusoma vitabu, hivyo ni muhimu
nyie wanafun zi kutumia maktaba hii kwa kusoma vitabu vingi zaidi kwani kuna
mambo mengi mazuri katika kujisomea na tuombe mashirika mengine ni
vyema yakajitokeza kuchangia maendeleo ya elimu nchini”Alisema Manase.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo,Georgia Mgashe,amefafanua kuwa
vitabu hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa shule hiyo kwani
hakutakuwa na kisingizio cha kukosekana kwa vitabu shuleni hapo .
“Imani yangu ni kwamba kwa sasa wanafunzi watasoma kwa bidii na kujituma
zaidi kwani hakuna kisingizio cha kukosekana kwa vitabu tumeona GGM wameweka
vitabu vingi katika maktaba yetu”Alisema Mgashe.
Msemaji wa Read internation Stella Mtega ,ametoa
shukrani kwa mgodi wa dhahabu wa GGM kwa kuwezesha ufadhili vitabu
vingi katika maktaba hiyo.
Akizindua Maktaba hiyo Mgeni rasmi ambae ni mkuu wa wilaya ya Geita mh
Herma Kapufi amewasisitiza wanafunzi kutunza vifaa na vitabu
vilivyonunuliwa ili viweze kuja kutumiwa na wanafunzi wengine.
No comments:
Post a Comment