Mhadhiri
wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria akielezea hali ya vyuo vikuu vya
Afrika katika muktadha wa Kimataifa wakati wa kongamano la kuazimisha miaka 55
toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya washiriki wa kongamano maalum la
kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wakimsikiliza kwa makini Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini
Nigeria wakati akielezea hali ya vyuo vikuu vya Afrika katika muktadha wa
Kimataifa mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akifurahia
jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) wakati wa
kongamano la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam mapema hii leo Chuoni hapo, katikati ni Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade
Aina toka nchini Nigeria.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Wakuu wa Vitivo wa
Chuo hicho wakati wa kongamano la kusherehekea kutimiza miaka 55 toka
kuanzishwa kwa chuo hicho.
Uongozi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) takiwa kuhakikisha Chuo hicho kinaendelea
kuwa kiongozi miongoni mwa Vyuo Vikuu nchini.
Ushauri huo umetolewa na Rais mstaafu wa awamu ya
Nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete alipokuwa akifungua maadhimisho ya miaka 55 ya chuo hicho leo
Jijini Dar es Salaam.
“Hiki ndicho Chuo kiongozi kati ya Vyuo Vikuu vyote
hapa nchini, mnatakiwa kuhakikisha kinaendelea kuwa kiongozi huku Vyuo vingine
vikifuatia”. Alisema Dkt. Kikwete
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Profesa Lwekaza Mukandara amesema kuwa pamoja na changamoto zinazo
kikabili chuo hicho wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kusaidia katika kuleta
maendeleo ya chuo hicho.
Alisema kuwa baadhi ya changamoto zimetatuliwa kwa
pamoja kati ya Serikali na wahisani ambapo alisema kuwa ujenzi wa kumbi mpya za
mihadhara, Maabara za Kisasa na jengo la malazi,pamoja na ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea katika
Kampasi ya Julius K. Nyerere ambayo itakuwa na uwezo wa kutumiwa na wanafunzi
4000 mara itakapo kamilika.
Akiwasilisha mada juu ya “hali ya Taaluma Barani
Afrika katika Muktadha wa Kimataifa” Mhadhiri wa Heshima kutoka nchini Nigeria,
Profesa Tade Aina amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni moja kati ya
Vyuo Vikuu mahiri barani Afrika ambapo kimetoa mchango mkubwa kwa ukombozi wa
nchi nyingi za bara hili.
Aliongeza kuwa yeye binafsi ni mnufaika mkubwa wa
UDSM kwani amekuwa na ushirikiano mkubwa na baadhi ya wahadhiri kutoka chuo
hicho katika masuala mbalimbali ya taaluma.
Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambaye pia alikuwa
Mwenyekiti wakati wa uwasilishaji mada alisema kuwa kipindi Chuo hiki
kinaanzishwa aina ya masomo yaliyokuwa yanafundishwa chuoni hapo yalikuwa na
muelekeo kuandaa wafanyakazi wa Serikali kwa wakati huo.
Na kuongeza kuwa muelekeo wa aina ya masomo
uliendelea kubadilika kadri ya siku zilivyokwenda kutokana na mabadiliko ya
teknolojia na uhitaji wa soko la ajira.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinaadhimisha miaka 55
tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1961 kikiwa ni tawi la Chuo Kikuu cha
London, ambapo awali kilianzia katika mtaa wa Lumumba kikiwa na wanafunzi 14
kabla ya kujengwa mahali kilipo sasa katika eneo la Mlimani.
No comments:
Post a Comment