Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu
(katikati) akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa Meneja Msaidizi TEMESA
Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma (kushoto) alipotembelea kituo
hicho, kulia ni Mhasibu wa TEMESA Tanga Bw. Lusenga David.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu
(kushoto aliyesimama) akizungumza na watumishi wa TEMESA Tanga
wakati alipotembelea kituo hicho kuangalia hali ya utendaji kazi, kulia ni
Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma.
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka wafanyakazi wa
kivuko cha Mv Tanga kuzingatia usalama wa abiria kwa kufata kanuni na Sheria za
usafirishaji wa abiria kupitia vivuko.
Amesema hayo
alipotembelea na kuongea na watumishi wa kivuko cha MV. Tanga
kinachosafiri kati ya Pangani na Bweni na kuwasisitiza watumishi hao juu ya
suala la usalama wa abiria na kuwa waaminifu katika ukusanyaji wa
mapato ya kivuko hicho.
Ndugu zangu hapa
tunabeba roho za watanzania wenzetu tuwe makini sana na kuzingatia Sheria na
taratibu zilizopo ili kuhakikisha usalama wa hawa abiria tunaowahudumia”
Alisisitiza Dkt Mgwatu.
Kwa upande wake Meneja
Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma amemuahakikishaia
Mtendaji Mkuu kuwa watazingatia taratibu na Sheria zilizopo ili kuhakikaisha
usalama wa abiria wanaowahudumi kupitia kivuko cha Mv Tanga na vivuko vingine
vilivyopo mkoani Tanga.
Aidha kwa upande wao
watumishi wa Mv Tanga wamemwaomba Mtendaji Mkuu kuwasaidia kutatua changamoto
mbalimbali zilizopo zikiwepo uhaba wa vifaa kwa ajili ya kutekeleza majukumu
yao ya kila siku.
Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo
kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo
ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huyo.
No comments:
Post a Comment