Serikali kupitia Mradi
wa Mpango wa Kuboresha Elimu – EQUIP (Education Quality Improvement Programme)
imeendelea kuboresha mfumo wa Elimu hapa nchini katika nyanja ya mitaala kwa
wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tatu, uongozi bora katika shule za msingi
pamoja na mifumo ya utoaji taarifa na takwimu sahihi.
Mratibu wa mradi huo
hapa nchini Bw Johan Bentinck, amesema hayo leo jijini, Dar es Salaam alipokuwa
akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo na namna ambavyo
umefanikiwa katika kuboresha Elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi
katika mikoa saba hapa nchini.
Mradi huo umetoa fursa
kwa walimu kupata mafunzo ya namna ya ufundishaji bora utakaomuwezesha
mwanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu kujua kusoma, kuandika na kuhesabu
ndani ya muda mfupi na kwa ufasaha.
Aidha kupitia mradi
huo ufundishaji darasa la Kwanza mpaka la Nne umeboreshwa ambapo mwanafunzi
anaweza kuunganisha maneno kwa kutumia sauti. Vile vile kumekuwepo na njia
nyingine za kufundisha kupitia nyimbo na michezo mbalimbali kwa wanafunzi wa
madarasa ya awali.
Pia mradi umewezesha
kuanzishwa kwa madarasa ya awali ambayo hayakuwepo katika shule za msingi
zilizoko vijijini. Wanafunzi wa madarasa hayo wamekuwa wakifundishwa na walimu
wa kujitolea kwa muda wa wiki 12 na baada ya hapo hujiunga na darasa la Kwanza.
Aidha mradi huo
umeleta mafanikio makubwa katika sekta ya Elimu hapa nchini ambapo kasi ya ya
kutamka maandiko kwa mwanafunzi wa darasa la Kwanza mpaka la Tatu ilikuwa 21.3
mwaka 2014 na sasa ni 30.0
“Mradi huo kwa sasa
unahusisha mikoa ya Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mara na Lindi
huku mikoa mingine miwili ya Katavi na Singida inategemea kuongezwa
mwaka 2017,” alifafanua Bentinck.
No comments:
Post a Comment