Shule ya sekondari Geita iliyopo Wilayani na Mkoani
geita ni moja kati ya shule ambazo zimeendelaea kuwa na changamoto nyingi moja
wapo ni wanafunzi kugoma, kuharibu,
miundombinu na hata kuwafanyia Fujo Walimu
Hali hii imempelekea mkurugenzi wa halmashauri ya mji
wa geita,mwandisi Modest Aporinali
kufika shuleni lengo ni kuzungumza na wanafunzi, uongozi, wa shule pamoja na
walimu shuleni hapo.
Kutokana na suala hili walimu wameanza kuelezea matatizo waliyonayo kama ambavyo wanavyofafanua hapa.
Aidha kutokana na maelezo hayo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
mji wa Geita,M odest Aporinali,
amekutana na wanafunzi na kutoa maagizo
ambayo wanafunzi wanatakiwa
kuhakikisha wanayatekeleza.
Mkurugenzi aporinali, ameongeza kuwa hatakuwa na
huruma kwa mwanafunzi ambae ataonekana
kwenda kinyume na kanuni na sheria zilizowekwa shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment