Baadhi
ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya
mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji
viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru
akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya
mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (katikati) akifuatilia
mada mbalimbali zilizowasilishwa na wadau mbalimbali wakati uzinduzi wa matokeo
ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar
es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kulia) akiteta jambo
na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Adelhelm Meru wakati wa uzinduzi wa matokeo
ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na wadau
mbalimbali wa maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati wa uzinduzi
wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016
Jijjini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya
mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika vitabu
mbalimnbali vya taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji
viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kushoto) akimkabidhi
taarifa ya kitabu cha utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani
ya mwaka 2013 kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia viwanda (UNIDO), Gerald Runyoro leo Oktoba 17, 2016 Jijjini
Dar es Salaam
Serikali imeitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
kwa kushrikiana na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Shirika la Maendeleo ya
Viwanda Duniani (UNIDO) na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kufanya
utafiti ili kubaini idadi na maendeleo ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini NA Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Dkt Charles Mwijage wakati wa uzinduzi wa matokeo ya
Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.
Dkt Mwijage alisema kuwa katika mataifa
yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na Singapore uchumi wa
nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi kutokana na kuweka mkazo
katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.
Alisema katika kuharakisha kasi ya maendeleo ya
vidogo yanapatikana nchini, Wizara yake imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania
kupendelea kujenga viwanda vidogo vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya
viwanda nchini kutaisaidia kuinua uchumi wa nchi.
“Asilimia 25- 40 ya mazao ya kilimo yanayovunwa
huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani, katika kukabiliana na hali hiyo
Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuwawezesha wakulima
wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi mazao yao” alisema Mwijage.
Aidha, Dkt Mwijage alisema, sekta ya viwanda vidogo
vidogo nchini imeendelea kukua kwa kasi nchini ambapo hadi sasa kuna jumla ya
viwanda 3800 vilivyoanzishwa nchini kuanzia Novemba 2015 hadi octoba, 2016.
Katika hatua hiyo Dkt Mwijage alisema kuwa Wizara
yake inaendelea kuhamasisha Sekta binafsi kuwekeza katika Sekta ya viwanda
vidogo, vya kati na vikubwa ikiwa jukumu kuu la Serikali ni kuhakikisha nchi
inakuwa salama na inajenga mazingira wezeshi kwenye sekta binafsi kuzalisha na
kufanya biashara.
Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Dkt Albina Chuwa alisema kuwa matokeo hayo yanaonyesha mafanikio katika sekta
ya viwanda ikiwemo kuongezeka kwa ajira zipatazo 264,223 nchini na kuchangia
uchumi kwa takribani Shilingi bilioni 8.0 kwa mwaka 2013.
Alisema kuwa Takwimu za matokeo ya sense ya
uzalishaji viwandani ni rasmi na kuwataka watunga sera, wanasiasa, viongozi,
sekta binafsi na watu binafsi kutumia
matokeo hayo kwa lengo la kuboresha Sekta ya viwanda nchini.
No comments:
Post a Comment